Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Kutangaza Fursa Za Uwekezaji Nchini Uingereza
Oct 06, 2026
Tanzania Kutangaza Fursa Za Uwekezaji Nchini Uingereza
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, aondoka nchini kuelekea Uingereza kwa ziara ya kikazi ya siku tano, ambapo atafungua Jukwaa la Uwekezaji la Tanzania na Uingereza
Na Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameondoka nchini kuelekea Uingereza kwa ziara ya kikazi ya siku tano, ambapo atafungua Jukwaa la Uwekezaji la Tanzania nchini humo.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu ataongoza ujumbe wa Tanzania katika kukutana na wadau, wawekezaji na viongozi wa kampuni mbalimbali zinazofanya shughuli katika sekta za madini, benki, teknolojia, usafirishaji na miundombinu, kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kutangaza fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania.

Jukwaa hilo litatoa fursa kwa Tanzania kutangaza vipaumbele vya Dira ya Maendeleo 2050 katika eneo la uwekezaji, pamoja na kueleza hatua zinazochukuliwa na Serikali kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Aidha, litahamasisha na kuwakaribisha wadau, wawekezaji na wafanyabiashara kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.

Jukwaa hilo pia linalenga kuvutia mitaji na teknolojia, kukuza ujuzi na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania, sambamba na kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya miundombinu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2050.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali, chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kuimarisha diplomasia ya uchumi, kuvutia uwekezaji na kusimamia utekelezaji wa sera za maendeleo kwa manufaa ya Watanzania.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor