Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tangazo kwa Umma
May 18, 2018
Na Msemaji Mkuu

TUME YA MADINI

TANGAZO KWA UMMA Tume ya Madini inapenda kuwatangazia wananchi na wadau wote wa Sekta ya Madini walioko nje na ndani ya Nchi kuwa: 1. Tume ya Madini imeanza zoezi la kuhakiki maombi ya leseni mbalimbali za madini kwa lengo la kutoa leseni hizo kwa maombi ambayo yatakidhi vigezo. 2. Tume imeanza zoezi hili kwa kupitia na kuhakiki maombi ya leseni yaliyokuwa yamewasilishwa Wizarani kabla ya tarehe 04/07/2017. Hata hivyo Tume inawahakikishia wadau wote kuwa maombi yaliyowasilishwa Wizarani baada ya tarehe hiyo (04/07/2017) nayo yatashughulikiwa ndani ya muda mfupi ujao. 3. Baada ya kupitia na kuhakiki maombi yaliyowasilishwa kabla ya tarehe 04/07/2017, Tume imeridhia kuwa leseni zifuatazo zitolewe kwa utaratibu ufuatao: i. LESENI ZITAKAZOTOLEWA NDANI YA JUMA MOJA KUANZIA TAREHE YA TANGAZO HILI. a) Leseni 1142 za Uchimbaji Mdogo (Primary Mining Licence - PMLs) ambazo zimeshalipiwa ada za kuandaa leseni. b) Leseni 399 za wafanyabiashara wa madini za aina ya “Brokers Licence” za kipindi kinachoishia Juni 2018. c) Leseni 150 za wafanyabiashara wa madini za aina ya “Dealers Licence” za kipindi kinachoishia Juni 2018.

ii. LESENI ZITAKAZOTOLEWA NDANI YA MWEZI MMOJA BAADA YA TANGAZO HILI. Leseni 3,252 za Uchimbaji Mdogo (PMLs) zitatolewa kwa wahusika baada ya waombaji hao kulipia ada za uandaaji wa leseni. Wahusika wanatakiwa kulipa ada hiyo ya uandaaji wa leseni ndani ya siku ishirini na nane (28) baada ya tangazo hili. Tume inasisitiza kuwa hizi leseni zitatolewa tu kwa wale waombaji watakaotimiza sharti hilo la malipo ya ada ya uandaaji wa leseni. Orodha ya maombi ya leseni yaliyopitishwa katika kifungi (i) na (ii) hapo juu inapatikana katika Ofisi za Madini za Kanda husika hivyo waombaji wa leseni hizo wanatakiwa kwenda kwenye ofisi za Kanda kwa maelekezo zaidi. iii. UTOAJI WA LESENI ZA KATI ZA UCHIMBAJI MADINI (MINING LICENCES – MLs) NA LESENI ZA UTAFUTAJI MADINI (PROSPECTING LICENCES – PLs) Tume imepitia pia maombi ya leseni za Uchimbaji wa Kati (Mining Licences – MLs) na Utafutaji wa Madini (Prospecting Licences – PLs) na kufikia uamuzi ufuatao: Leseni za Uchimbaji wa Kati (MLs) a) Leseni 8 za Uchimbaji wa Kati zilizokidhi vigezo zitolewe. b) Leseni 7 za Uchimbaji wa Kati zitolewe baada ya waombaji husika kukamilisha michakato ya kisheria kuhusiana na leseni zao (amalgamation of PMLs and conversion to MLs as well as Resolutions of Pending Disputes). Leseni za Utafutaji Madini (PLs) a) Leseni 88 za Utafutaji Madini (PLs) ambazo zimeshalipiwa ada za utayarishaji wa leseni zitolewe kwa waombaji. b) Leseni 62 za Utafutaji Madini (PLs) zitolewe baada ya waombaji kukamilisha malipo ya ada ya utayarishaji wa leseni husika. Pamoja na kuridhia utoaji wa leseni za Uchimbaji wa Kati (15) na za Utafutaji Madini (150) zilizoainishwa kwenye kifungu (iii) cha tangazo hili, Tume inawakumbusha waombaji wa leseni hizo kuwa wanatakiwa kuwasilisha kwa mujibu wa sheria maandiko maalumu yanayoainisha mipango yao ya Ushiriki wa Wazawa na utoaji huduma kwa Jamii (Local Content) ikijumuisha mipango ya wajibu wa Kampuni kwa Jamii (Corporate and Social Responsibilities) pamoja na Tamko la Kiapo cha Uadilifu (Integrity Pledge). Tume inasisitiza kuwa hakuna leseni hizi kubwa itakayotolewa bila muombaji kutekeleza na kukamilisha matakwa hayo ya kisheria. Orodha ya maombi ya leseni hizi Kubwa na za Kati yaliyopitishwa inapatikana katika Ofisi za Wizara ya Madini, Dodoma hivyo waombaji wa leseni hizo wanatakiwa kwenda kwenye ofisi Wizara kwa maelekezo zaidi.

Prof. Idris Suleiman Kikula MWENYEKITI WA TUME YA MADINI 18 Mei, 2018.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi