Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TANAPA Yatenga Bilioni 3.9 Kuendeleza Hifadhi Zilizopandishwa Hadhi
Aug 24, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Lusungu Helela - Kagera

Bodi ya Wadhamini ya Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) imeidhinisha na kuruhusu matumizi  ya bajeti ya mpito ya kiasi cha shilingi 3.9 bilioni ili zitumike kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi, uendelezaji utalii pamoja na ujenzi wa miundombinu katika Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa.

Hatua hiyo imekuja kufuatia tangazo la Serikali la kuyapandisha  hadhi Mapori ya Akiba ya Bihalamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa  kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamisi Kigwangalla wakati  alipokuwa akihitimisha  Bajeti ya Wizara mwezi Mei  mwaka huu Bungeni mjini Dodoma.

Mkuu wa Hifadhi, Damian Saru amesema hayo jana  mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga  wakati alipotembelea  mapori ya Biharamulo, Burigi na Kimisi (BBK) ikiwa ni  ziara yake ya  kikazi ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika  mapori hayo.

Alitaja fedha hizo kuwa  zimeshaanza kutumika katika kuimarisha ulinzi, kujenga miundo mbinu ya utalii na Utawala, kuainisha mipaka , kusimamia mchakato wa kupandisha hadhi mapori

Damian Saru, Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na TANAPA, aliwasilisha taarifa hiyo pamoja na kumweleleza Naibu Waziri huyo hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika mapori hayo.

Alimweleza kuwa askari 58 wameshafika kwenye mapori hayo matano kwa ajili ya kuongeza nguvu.

Mashine ya kutengeneza barabara ' Motor Grader moja imeletwa kwa sjiki ya kutengeneza barabara.

Pia, alimweleza Naibu Waziri huyo ikiwemo vitendea kazi ikiwemo ndege moja magari manne, mahema silaha, GPS vimeletwa katika mapori hayo kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi.

Kufuatia utekelezaji huo, Mkuu mwenye hadhi ya Mkuu wa Hifadhi alitaja mafanikio yaliyopatikana katika kIpindi kifupi cha utekelezaji maagizo hayo kuwa katika kipindi cha wiki mbili pamoja na ng'ombe 41 kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Pia , alitaja idadi ya watuhumiwa 12 wa ujangili wamekatwa.

Aidha, Saru alitaja aina za vifaa vilivyokatwa kuwa ni mitumbwi mitatu, mkaa gunia mbili pamoja na baiskeli zopatazo 10.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Mhe. Hasunga ameridhishwa na hatua ya TANAPA kwa ushirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa nzuri waliyoifanya.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi