Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tamasha la JAMAFEST Lasaidia Kukuza Ushirikiano wa Kikanda
Sep 06, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Eleuteri Mangi - WUSM

Tanzania inashiriki Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) 2022 ambalo linafanyika nchini Bujumbura Burundi likiongozwa na Kaulimbiu “Kutumia Rasilimali za Kiutamaduni kukabiliana na Athari za UVIKO-19 kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki”.

Akifungua tamasha hilo Septemba 5, 2022 katika Uwanja wa Intwari Bujumbura nchini humo, Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye amewashukuru Wakuu wa nchi za jumuiya hiyo kufanikisha vikundi vya Utamaduni na Sanaa kushiriki Tamasha la JAMAFEST 2022 kwa mafanikio nchini Burundi.

“Tukio hili husaidia sio tu ubadilishanaji wa kisanii na kitamaduni, lakini pia hukuza ushirikiano wa kikanda. Kuweza kuandaa tamasha hili la Sanaa na Utamaduni nchini Burundi, ni dalili tosha kwamba UVIKO-19 ipo nyuma yetu ushahidi kwamba Jumuiya yetu ni thabiti na kwa pamoja tunaweza kukabiliana na changamoto yoyote”, amesema Rais Mhe. Ndayishimiye.

Awali, akiwakaribisha washiriki wa tamasha hilo, Rais Mhe. Ndayishimiye,amesema washiriki kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki watafurahia sio tu hewa ya Burundi bali watafurahia madhari nzuri ya Ziwa Tanganyika, kula samaki aina ya migebuka, dagaa na kuhe ambao wanapatikana katika ziwa Tanganyika.

Aidha, Rais Mhe. Ndayishimiye amesisitiza umuhimu wa Tamasha hilo na kusema kuwa linanaongeza kuimarisha umoja na muingiliano kati ya watu wa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tamasha la JAMAFEST linafanyika kwa mzunguko ambapo mwaka 2022 ni zamu ya nchini Burundi baada ya kufanyika tamasha la 4 kufanyika kwa mafaniko makubwa jijini Dar es Salaam 2019.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi