Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TAGCO na Idara ya Habari- MAELEZO Zawezesha Utatuzi wa Changamoto Kada ya Mawasiliano Serikalini
Jun 28, 2019
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_44744" align="aligncenter" width="750"] Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mhandisi Victor Seif akisisitiza kuhusu umuhimu wa hatua zinazochukuliwa na dara ya Habari- MAELEZO na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa Umma hasa katika kipindi hiki miradi mikubwa inayolenga kuwakwamua wananchi kiuchumi inapotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.[/caption]

Na Frank Mvungi- Dodoma

Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wa Taasisi na Mashirika ya Umma  Jijini Dodoma wamekipongeza Chama Cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini TAGCO kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO kwa kuendelea kusimamia vyema kada ya Mawasiliano Serikalini.

Wakizungumza wakati wa ziara  ya ujumbe wa Chama hicho na Idara ya Habari  MAELEZO  kutembelea na kujionea changamoto zinazowakabili  ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili, Maafisa hao akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bw. Ntambi Bunyanzu amesema kuwa utaratibu huo unapaswa kuendelezwa ili kusaidia kuimarisha utendaji wa vitengo vya mawasiliano Serikalini.

“Utaratibu huu  wa kutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini unatoa fursa ya kubaini changamoto zinazokabili vitengo vya mawasiliano serikalini katika Taasisi zetu na unawezwesha kupatikana kwa suluhisho la changamoto hizo hivyo tunaomba uendelezwe” Alisisitiza Bunyanzu.

[caption id="attachment_44745" align="aligncenter" width="750"] Makamu Mwenyekiti wa Chama cha MaafisaMaafisaHabarinaMawasilianoSerikalini (TAGCO) Bi Sarah Kibonde akisisitiza umuhimu wakuimarisha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma wakati wa ziara ya ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari- MAELEZO katika Ofisi za Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Jijini Dodoma ili kujionea utendaji wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.[/caption]

Akifafanua amesema kuwa amefarijika kuona kuwa utaratibu wa kutembelea Vitengo hivyo umekuwa endelevu na kwa kipindi hiki utasaidia kuendelea kuimarisha mawasiliano Serikalini kama ilivyo azma ya Serikali.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dodoma Bw.  Sebastian Warioba amesema kuwa vitengo hivyo vina jukumu kubwa katika kuimarisha mawasiliano Serikalini ili hatimeye wananchi waweze kufahamu yale yote yanaytotekelezwa na Serikali.

“ Tunalo jukumu kubwa la kuendelea kuimarisha mawasiliano serikalini kama Maafisa habari  na Mawasiliano Serikalini hivyo nawahamasisha  wenzangu tuendelee kujituma na kushirikiana na viongozi wetu katika kutoa taarifa kwa umma kuhusu miradi ya maendeleo.” Alisisitiza Warioba

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bi Sarah Kibonde amesema kuwa maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wanapaswa kufanya kazi kimkakati na kuepuka mazoea. [caption id="attachment_44746" align="aligncenter" width="750"] Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bi Sarah Kibonde akisisitiza jambo kwa mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Bw. Sebastian Warioba leo June 24, 2019.[/caption]

“ Tunalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa tunatangaza mafanikio ya Serikali hasa miradi mikubwa ya kimakakati inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayolenga kuwaletea wananchi maendeleo” Alisisitiza

Akifafanua amesema kuwa Chama hicho kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO wataendelea kufanya ufuatiliaji wa utendaji wa maafisa Habari Serikalini ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa weledi.

Ziara ya Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini na Idara ya Habari MAELEZO imeanza June 24 , 2019  na inatarajiwa kukamilika June 29, 219 ikishirikisha Taasisi  na Mashirika ya Umma yaliyopo Jijini Dodoma, Baadhi ya Taasisi za zilizotembelewa ni pamoja  DUWASA, Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA).

[caption id="attachment_44747" align="aligncenter" width="750"] Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Casmir Ndambalilo akisisistiza umuhimu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini katika Mamlaka na Taasisi za Serikali kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika leo Jijini Dodoma ili kujionea utendaji wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Tume hiyo.[/caption] [caption id="attachment_44748" align="aligncenter" width="750"] Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bi Sarah Kibonde (katikati) akifuatilia maelezo  ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bw. Ntambi Bunyanzu  wakati wa ziara ya ujumbe wa chama hicho  na Idara ya Habari MAELEZO katika Ofisi za Tume hiyo.[/caption] [caption id="attachment_44749" align="aligncenter" width="750"] Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini Mhandisi Victor Seif (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari- MAELEZO walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma leo June 24, 2019.[/caption] [caption id="attachment_44751" align="aligncenter" width="900"] Katibu Mkuu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Abdul Njaidi akisisitiza mikakati ya kuimarisha Mawasiliano Serikalini katika Taasisi na Mashirika ya Umma leo Jijini Dodoma wakati wa ziara ya ujumbe wa Chama hicho na Idara ya Habari- MAELEZO walipotembelea Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) leo June 24, 2019.[/caption]

Muwakilishi  wa  Mkurugenzi  wa  Idara  ya  Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu  wa  Serikali Bw. Casmir  Ndambalilo  akiagana na  mkuu  wa Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini wa  Mamlaka ya Maji Safi  na  Usafi  wa Mazingira Dodoma (DUWASA)  Bw. Sebastian Wariobaleo June 24, 2019 mara baada ya  ziara  ya ujumbe  huo leo  Jijini Dodoma.

(Pichana Frank Mvungi)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi