Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TAGCO, Idara ya Habari-MAELEZO Zapongezwa Kwa Utendaji
Jul 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33915" align="aligncenter" width="900"] Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akisisitiza jambo kwa ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashauri hiyo kukagua na kujionea jinsi maafisa Habari wanavyotekeleza jukumu la kuisemea Serikali katika Mikoa na Halmashuri zao.[/caption] [caption id="attachment_33916" align="aligncenter" width="900"] Kiongozi wa Ujumbe wa Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Gaudensia Simwanza akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashuri hiyo uliolenga kukagua na kuweka mikakati ya pamoja katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma.[/caption]

Frank Mvungi- MAELEZO, Tunduru

Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) vimepongezwa kwa kubuni na kuweka utaratibu wa kufuatilia utendaji wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini hadi katika ngazi ya Halmashuri.

Akizungumza na Ujumbe wa chama hicho uliofika Ofisini kwake mapema wiki hii, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw.  Chiza Marando  amesema kuwa hili ni jambo la kihistoria ambapo ufuatiliaji wa utendaji wa Maafisa Habari unafanyika katika ngazi zote.

“Tangu nimeanza kazi sijawahi kushuhudia ufuatiliaji wa namna hii na sisi tuko tayari wakati wote kutoa ushirikiano utakaosaidia Afisa Habari katika Halmashauri yetu atekeleze majukumu yake vizuri hasa katika kutangaza miradi ya maendeleo” Alisisitiza Marando

[caption id="attachment_33917" align="aligncenter" width="900"] Mwakilishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akisisitiza umuhimu wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kuwajibika katika kuisemea Serikali hasa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mikoa na Halmashuri zao, hiyo ilikuwa katika ziara iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO.[/caption] [caption id="attachment_33918" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akisisitiza kuhusu namna Halmashuri hiyo ilivyojipanga katika kuimarisha mawasiliano ya kikakati hasa kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.[/caption]

Akifafanua Bw.  Marando amesema kuwa Halmashuri yake inatambua umuhimu wa mawasiliano kati ya Serikali na Wananchi hivyo imeweka kipaumbele katika kuwezesha  utoaji wa taarifa za maendeleo kwenda kwa wananchi ili waweze kushiriki katika kujiletea maendeleo.

Kwa  upande wake Kiongozi wa Msafara wa Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini  (TAGCO) na Idara ya Habari – MAELEZO Bi. Gaudensia  Simwanza amesema kuwa Maafisa Habari wanalo jukumu kubwa katika Halmashauri na Mikoa katika kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao.

[caption id="attachment_33919" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akiagana na Bw. Casmir Ndambalilo kutoka Idara ya Habari MAELEZO na ujumbe wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) mara baada ya ujumbe huo kukamilisha ziara katika Halmashauri hiyo mapema wiki hii.[/caption]

Aliongeza kuwa  kutokana na jukumu hilo wanapaswa kutumia rasilimali zilizopo kutekeleza jukumu hilo kwa weledi.

Ziara ya Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini na Idara ya Habari MAELEZO inafanyika katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kufuatilia na kuona utendaji wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini katika ngazi zote ili kutoa msukumo na kuweka mikakati ya pamoja katika kuimarisha Mawasiliano ya Serikali kwa umma ili kuchochea maendeleo na ustawi wa wananchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi