Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TADB, Tume ya Umwagiliaji Wajipanga Kuchagiza Kilimo cha Umwagiliaji
Sep 25, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_35648" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere (kulia) wakitia saini makubaliano yanayolenga Kuimarisha Uendelezaji wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini.[/caption]

Katika kutekeleza kwa vitendo jukumu la kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia makubaliano na Tume ya Umwagiliaji ya Taifa (NIRC) ili kuchagiza kilimo cha umwagiliaji nchini.

Akizungumza wakati wa utiaji wa saini wa makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine alisema benki imejipanga kuchagiza tasnia ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo.

“Ili kuninua uzalishaji wenye tija katika sekta ya kilimo nchini benki imejipanga kuwekeza mtaji wa kutosha katika kilimo cha umwagiliaji,” alisema.

Bw. Justine aliongeza kuwa mpaka sasa TADB imeshatoa mkopo katika miradi 9 mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere alisema tasnia ya umwagiliaji ina mchango mkubwa katika kunyanyua uzalishaji nchini hatahivyo muitikio finyu wa wadau umekuwa ukirudisha nyuma tasnia hiyo.

[caption id="attachment_35649" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere (kulia) wakionesha makubaliano hayo.[/caption]

Mhandisi Dkt. Matekere ameishukuru TADB kwa kuwa taasisi ya kwanza ya kifedha kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji.

“uwekezaji huu wa pamoja utasaidia kuongeza uzalishaji hali itakayowaongezea kipato wakulima nchini na hivyo kusaidia kupunguza umaskini wa kipato kwa wakulima hasa wanaolima kwa kutegemea mvua,” alisema.

Makubaliano hayo, yamelenga kuweka mfumo wa ushirikiano  kati ya TADB na NIRC katika kuanzisha na kuimarisha Jumuiya za Umwagiliaji na vyama vya wakulima ili kwenda sambamba na Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji na Kanuni zake kwa miradi ya kilimo iliyochaguliwa.

Pia, yamelenga katika kubaini na kuijengea uwezo miradi ya umwagiliaji ili kuweza kuipatia mikopo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji nchini.

Kwa mujibu wa taarifa za hali ya umwagiliaji nchini, miundombinu ya umwagiliaji iliyoboreshwa inachachochea uzalishaji katika kilimo kutoka tani 1.8 kwa hekta kwa kilimo cha kawaida hadi tani 5 kwa hekta kwa kilimo kinachotegemea umwagiliaji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi