Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TADB, NABAD na MIVARF Wazinoa Taasisi za Fedha
Jun 12, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_3355" align="aligncenter" width="630"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) akifungua Mafunzo ya Awali ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo. Wanaomsikiliza ni wadau kutoka mabenki na taasisi za kifedha nchini. Mafunzo hayo ya siku sita yanaendeshwa kwa pamoja kati ya TADB, NABAD na MIVARF.[/caption]

Na Mwandishi Wetu,

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na  Benki ya Taifa ya Kilimo na Maendeleo Vijijini India (NABAD) na Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) zimeanza kutoa Mafunzo ya Awali ya Kanuni za ukopeshaji katika kilimo.

[caption id="attachment_3359" align="aligncenter" width="630"] Meneja Msaidizi wa Mafunzo kutoka NABAD, Dkt. R.S. Reddy akizungumza kuhusu mafunzo hayo. Mafunzo hayo ya siku sita yanaendeshwa kwa pamoja kati ya TADB, NABAD na MIVARF.[/caption] [caption id="attachment_3364" align="aligncenter" width="630"] Meneja Msaidizi wa Mafunzo kutoka NABAD, Bw. M.R. Gopal akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mafunzo ya Awali ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo. Mafunzo hayo ya siku sita yanaendeshwa kwa pamoja kati ya TADB, NABAD na MIVARF.[/caption]

Mafunzo hayo ya siku sita yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma hasa kutoka mabenki na taasisi za kifedha nchini kuweza kutoa huduma kwa wakulima kwa wakati na kuzingatia tija kwa wakulima nchini ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo.

Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa TADB alisema kuwa katika kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini Tanzania, TADB imeamua kuwajengea uwezo wadau kutoka mabenki na taasisi za kifedha nchini kwa kushirikiana na  NABAD na MIVARF ili kuweza kutoa huduma kwa uhakika ili kuwakomboa wakulima nchini.

[caption id="attachment_3365" align="aligncenter" width="630"] Washiriki wa Mafunzo ya Awali ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa mafunzo hayo. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hoteli ya Beach Comber, jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_3366" align="aligncenter" width="630"] Mshauri wa Kiufundi wa MIVARF, Bw. Ravi Malik (kushoto) akimkabidhi zawadi kutoka NABAD Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia).[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi