Ikulu, Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Joseph Constantine Mafuru kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Mkoani Dodoma.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mafuru alikuwa Mkuu wa Idara ya Ardhi, Mipango Miji na Maliasili wa Jiji la Dodoma.
Bw. Mafuru anachukua nafasi ya Bw. Godwin Kunambi.
Uteuzi wa Bw. Mafuru unaanza leo tarehe 19 Agosti, 2020.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino
19 Agosti, 2020