Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;
Kama tulivyojulishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwamba Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, amefariki jana tarehe 29 Februari, 2024 saa 11.30 Jioni katika Hospitali ya Mzena,
kwa masikitiko makubwa, ninaomba kuungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa Salamu za Pole kwa Mheshimiwa Dr Hussein Ali Hassan Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, wanafamilia na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa wa kiongozi wetu mpendwa.
Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;
Kufuatia msiba huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametangaza maombolezo ya siku saba na bendera kupeperushwa nusu mlingoti kuanzia leo tarehe 1 Machi, 2024. Katika kipindi hiki cha siku saba za maombolezo, Taifa litaungana kwa pamoja na wanafamilia katika maombolezo na mazishi ya Kitaifa yatakayofanyika huko Unguja Zanzibar kwa ratiba ifuatayo;.
Milango ya uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kwa ajili ya Wananchi kuingia kwa ajili ya maombolezo.
Viongozi mbalimbali kuwasili uwanja wa Uhuru kwa ajili ya Maombolezo ya Kitaifa na Kuaga mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi
Mwili wa Hayati Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi kuondoka nyumbani Mikocheni kuelekea Msikiti Mkuu wa BAKWATA uliopo Kinondoni ambako Sheikh Dokta Abubakar Bin Zuber Bin Ali ataongoza swala ya Ijumaa pamoja na taratibu zote za kidini.
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi kuelekea Uwanja wa Uhuru.
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, kuondoka uwanja wa Uhuru kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere;
Wananchi wa Jiji la Zanzibar na maeneo mengine ya Unguja kupokea Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume na kuelekea nyumbani kwa marehemu.
Milango ya uwanja wa Amani itakuwa wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi ambako Shughuli ya kitaifa itafanyika.
Viongozi mbalimbali kuwasili uwanja wa Aman kwa ajili ya Maombolezo ya Kitaifa na Kuaga mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi kuondoka nyumbani kwa marehemu kuelekea Uwanja wa Aman.
Dua na swala kutoka kwa viongozi wa dini
Viongozi na Wananchi mbalimbali kutoa heshima za mwisho
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi uwanja wa Aman kuelekea kijijini kwa marehemu Mangapwani kwa ajili ya mazishi ya Kitaifa
Wananchi na Viongozi mbalimbali kushiriki Mazishi ya Kitaifa ya hayati Ali Hassan Mwinyi eneo la Mangapwani.
Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;
Watanzania tumepokea taarifa za msiba wa mzee wetu, kiongozi wetu Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa masikitiko makubwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametutaka Watanzania wote kuwa watulivu na wastahimilivu kutokana na kifo cha mpendwa wetu.
Ndugu Wananchi na watanzania wenzangu; pamoja na taarifa hii, Serikali itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu matukio ya kila hatua kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali.
INNA LILAHI WA INNA ILAYHI RAJI’ UN
SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA