Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Fidelice Mbaruku Simbagungile Mafumiko kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.
Uteuzi wa Dkt. Mafumiko umeanza leo tarehe 03 Aprili, 2018.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Mafumiko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW)
Dkt. Mafumiko anachukua nafasi ya Prof. Samuel Manyele ambaye amemaliza muda wake.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Aprili, 2018