Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taarifa kwa Umma
Oct 20, 2017
Na Msemaji Mkuu

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

Ofisi ya Msajili wa NGOs inapenda kuujulisha umma kuwa imesimamisha shughuli za Shirika la COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY (CHESA) kuanzia tarehe 20 Oktoba, 2017 ili kupisha uchunguzi unaofanywa dhidi ya tuhuma za shirika tajwa kujihusisha na uhamasishaji wa vitendo vya ndoa za jinsia moja katika maeneo mbalimbali nchini. Shirika tajwa pamoja na tuhuma mbalimbali zilizopo, linatuhumiwa kuratibu warsha kuhusu masuala ya ndoa za jinsia moja tarehe 17 Oktoba, 2017 katika hoteli ya Peacock, Ilala – Dar es Salaam. Kwa taarifa hii uongozi wa Shirika unaagizwa kusimamisha shughuli zake zote ikiwa ni pamoja na kufunga ofisi zote za Shirika hadi uchunguzi utakapokamilika. Ikumbukwe kuwa ndoa za jinsia moja hazikubaliki nchini kwani ni kinyume na mila, desturi na sheria za nchi.

M.S. Katemba

MSAJILI WA NGOs

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi