Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mtangazaji nguli, Marehemu Isaac Gamba aliyefariki jana nchini Ujerumani.
Dkt. Mwakyembe amemuelezea marehemu Isaac kuwa ni mmoja wa watangazaji mahiri nchini ambaye amekuwa akifanya kazi zake kwa weledi na kujituma katika vyombo mbalimbal vya habarii vikiwemo Redio Free Africa, Redio Uhuru, ITV na Radio One na baadae Redio Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) idhaa ya Kiswahili.
Waziri Mwakyembe ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, uongozi wa Redio Deutsche Welle pamoja na wana tasnia nzima ya habari kwa kuondokewa na mpendwa wao.
Imetolewa na
Shamimu Nyaki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
19/10/2018