Upimaji wa Magonjwa ya Moyo na Utoaji wa Elimu ya Afya ya Moyo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha Wahariri na Waandishi wa Habari kwamba katika kuadhimisha siku ya moyo Duniani itafanya uzinduzi wa upimaji wa afya ambao utaenda sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya afya ya moyo bila malipo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari wote pamoja na watoto wao. Upimaji huo utafanyika tarehe 28/09/2018 kuanzia saa nne (4) asubuhi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete. Usikose kuhudhuria nafasi hii muhimu ya upimaji wa afya. Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inasema: “Kwa moyo wangu, kwa moyo wako, sote pamoja kwa mioyo yetu , tunatimiza ahadi”.
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
27/09/2018