Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taarifa kwa Umma
Sep 24, 2018
Na Msemaji Mkuu

Ikulu, Dar es Salaam.

Kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba, 2018 katika ziwa Victoria, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

Bodi hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti wake Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri imevunjwa kuanzia leo tarehe 23 Septemba, 2018 wakati kamati ya uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea na uchunguzi wa ajali hiyo.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

23 Septemba, 2018

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi