MAANDALIZI YA MICHEZO YA SHIMIWI 2018
Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) limeandaa Michezo kwa Watumishi wa Seriali kutoka katika Wizara, Idara Zinazjitegemea, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa itakayofanyika Jijini Dodoma kuanzia tarehe 25 Septemba hadi 06 Oktoba, 2018 katika Viwanja vya Jamhuri na Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).
Michezo hiyo itakayoshindaniwa ni Mpira wa Miguu (Wanaume), Netiboli (Wanawake), Kuvuta Kamba (Wanaume na Wanawake), Riadha (Wanaume na Wanawake), Baiskeli (Wanaume na Wanawake), Karata (Wanaume na Wanawake), Bao (Wanaume na Wanawake), Drafti (Wanaume na Wanawake) na Darts (Wanaume). Usajili wa Wachezaji watakaoshiriki katika michezo hiyo tayari umeshaanza tarehe 1 Agosti, 2018 na utamalizika leo 31 Agosti, 2018. Vilabu vinaendelea kuthibitisha ushiriki wao kwa kutaja aina ya Michezo watakayoshiriki zoezi ambalo litafungwa ifikapo tarehe 15 Septemba, 2018.
Ratiba ya michezo ya Ufunguzi ni kama ifuatavyo:-
Kamba Wanaume: Bingwa mtetezi Ofisi ya Rais Ikulu vs MSD.
Kamba wanawake: Bingwa mtetezi RAS Iringa vs Viwanda.
Mpira wa Miguu: Bingwa mtetezi Wizara ya Elimu vs Ukaguzi (NAO).
Netboli: Bingwa mtetezi Menejimenti ya Utumishi wa Umma vs RAS Manyara.
Shirikisho linaviomba Vilabu vyote kujianda kikamilifu na kukamilisha taratibu za ushiriki mapema ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima. Aidha, tunawaomba wananchi wote wakazi wa Jiji la Dodoma kujitokeza kwa wingi viwanjani kushuhudia Michezo hii ambayo kwa mara ya mwisho katika Mkoa huu ilifanyika mwaka 2013. Hii ni burudani pekee iliyoandaliwa kwa ajili ya wakazi wa Jiji la Dodoma.
Imetolewa leo Tarehe 31 Agosti, 2018 0754 - 763140
Moshi Y. Makuka
KATIBU MKUU – SHIMIWI