Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Jen. Mstaafu Davis Mwamunyange kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
Jen. Mstaafu Mwamunyange ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Mstaafu.
Uteuzi wa Jen. Mwamunyange unaanza leo tarehe 07 Julai, 2018.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
07 Julai, 2018