Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Startimes, Sibuka Kudhamini Ligi ya Kikapu.
Aug 04, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_8377" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Mpira wa kikapu Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Okare Emesi (kulia) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini waliopata toka kampuni ya Startimes na Sibuka mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa chama hicho Bw. Peter Mpangala na kushoto ni Afisa Mahusiano toka Startimes Bw. Samwel Gisayi.[/caption]

Na Agness Moshi

Kampuni ya kurusha matangazo kwa njia ya digitali na waauzaji wa ving’amuzi Startimes na Shirika la utangazaji la Sibuka waidhamini ligi ya mpira wa kikapu Dar es Salaam (RBA).

Hayo yamesemwa na Afisa Mahusiano wa Startimes Bw. Samuel Gisayi wakati akitambulishwa na Chama Cha Mpira wa Kikapu (BD) kwa waandishi wa habari  kuwa  mdhamini mpya  wa RBA, Jijini Dar es Salaam.

Bw. Gisayi amesema kuwa udhamini kwa ligi hiyo kwa sasa ni  wa muda mfupi, na baada ya kumalizika kwa ligi ya RBA wako kwenye mazungumzo ya kuwa wadhamini wa mojakwa moja wa mchezo huo kwa kipindi cha miaka mitano.

[caption id="attachment_8380" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Masoko wa chama hicho Bw. Peter Mpangala (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini waliopata toka kampuni ya Startimes na Sibuka mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Okare Emesi na kushoto ni Afisa Mahusiano toka Startimes Bw. Samwel Gisayi.(Picha Eliphace Marwa.)[/caption]

“Tumeamua kudhamini RBA ili kukuza vipaji vya wacheza mpira wa kikapu kwa sababu Makampuni mengi yamekua yakiwekeza kwenye mpira wa miguu na kusahau mchezo huu kusaidia wachezaji waweze kuonekana na kusajiliwa kwenye timu kubwa” , alisema Bw.Gisayi.

Bw.Gisayi ameongeza kuwa tayari wamefanya mambo mbalimbali ili kuweza kufanikisha mashindano hayo ikiwemo kuboresha viwanja ambavyo mchezo huo utafanyika na kudhamini gharama zote za uendeshaji wa ligi hiyo kuanzia mzunguko wapili mpaka fainali.

“Ukiachana na uuzaji wa ving’amuzi Startimes inashirikiana na Jamii katika kuleta maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo michezo ili kuinua vipaji vya Watanzania” ,alisititiza Bw.Gisayi.

Bw.Gisayi ametoa wito kwa wafanyabiashara kupeleka matangazo yao kwenye vituo vyao ili waweze kutangaziwa kwa bei rahisi wakati wa ligi hiyo , pia ametaka wadau mbalimbali kutoa ushirikiano kwa  mchezo wa mpira wa kikapu kama michezo mingine .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa habari na Mawasiliano Bw.Peter Mpangala amesema kuwa wanaimani mchezo huo utafika mbali  na utakua wa kibiashara kupitia udhamini wa startimes na sibuka kwasababu wamepata kupata fursa ya kuwa na kurusha michezo yao mubashara kwenye televisheni.

“Ukiwa na kipindi kwenye televisheni unakaribisha wadau wengi zaidi kuudhamini mchezo na tunategemea biashara kubwa kwa wachezaji”, alisema Bw.Mpangala.

Bw.Mpangala ameongeza kuwa amefurahishwa na kitendo cha startimes kuwadhamini kwa sababu kupitia kampuni hiyo ambayo inashirikiana na taasisi ya kubwa inayosimamia mchezo huo Duniani  (FIBA) wataweza kufikia malengo ya kuufikisha mchezo huo mbali.

Naye ,Mwenyekiti wa  Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Okare Emesu  amesema kuwa, wana mikakati ya pamoja na wadhamini hao ili kuufanya mchezo huo uwe wa kibiashara na uweze kufika mbele zaidi, vilevile ametoa wito kwa wananchi kufuatilia vipindi vya mchezo huo vitavyoonyeshwa kwenye king’amuzi cha startimes kupitia Tv Sibuka kila siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili saa kumi na mbili jioni.

Ligi ya RBA kwa sasa ipo kwenye mzunguko wa pili  na baada ya wiki 3 hatua ya  mtoano (playoff) itaanza rasmi kuelekea fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu Uwanja wa Taifa .

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi