Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Sirro Asisitiza Ushirikiano Kuondoa Uhalifu
May 29, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_1919" align="aligncenter" width="683"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvisha cheo kipya Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro wakati wa hafla ya kumuapisha kwake leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. IGP Sirro amechukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine. (Picha na: Frank Shija)[/caption]  

Na Jacquiline Mrisho 

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amewasisitiza wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kutoa taarifa za wahalifu waliopo katika maeneo yao jambo ambalo litapunguza au kuondoa kabisa uhalifu nchini. IGP Sirro ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokuwa  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi la Tanzania. [caption id="attachment_1920" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Jeshi la Polis Tanzania (IGP), Simon Sirro akila kiapo mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kuapishwa kwake kuwa IGP leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Uapaisho huo umefuatia uteuzi wa Rais ulifanyika jana tarehe 28 Mei kushika wadhifa huo kujaza nafasi iliyoacha wazi na Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi.[/caption] Amesema kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kulinda na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao hivyo ni wajibu wa jeshi hilo kuhakikisha nchi nzima ina ulinzi wa kutosha utakaopelekea wananchi kuishi kwa amani na utulivu na kuwawezesha kufanya kazi zao bila kubugudhiwa. “Uhalifu hauwezi kupungua kwa kutegemea Jeshi la Polisi pekee bali tunahitaji nguvu ya pamoja ili kushinda vita hiyo, ushirikiano wa wananchi unahitajika kwa kiasi kikubwa”,Alisema IGP Sirro. [caption id="attachment_1921" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro akiweka saini katika hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa kuwa IGP leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Upaisho huo umefuatia uteuzi wa Rais ulifanyika jana tarehe 28 Mei kushika wadhifa huo kujaza nafasi iliyoacha wazi na Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine. Wanaoshuhudia zoezi hilo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (wapili kushoto).[/caption] Ameongeza kuwa kipaumbele cha kwanza katika utendaji wake kwenye  nafasi hiyo ni kupambana na uhalifu pamoja nidhamu ya watendaji kazi kwani bila nidhamu, kazi ya kupambana na wahalifu haiwezi kufanikiwa. Aidha, amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Pwani ambao umekuwa na mauaji na uhalifu wa mara kwa mara kuwa atafanyia kazi changamoto zinazowakabili na  kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwa amani na utulivu. [caption id="attachment_1924" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya kiapo wakati wa hafla ya kumuapisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro (kulia) leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. IGP Sirro amechukua nafasi ya Ernest Mangu atakayepangiwa kazi nyingine.[/caption] [caption id="attachment_1927" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro (kulia) mara baada ya kumuapisha leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. IGP Sirro amechukua nafasi ya Ernest Mangu atakayepangiwa kazi nyingine. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi.[/caption]   [caption id="attachment_1931" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro akila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kinachotolewa na Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika hafla ya uapisho wake leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_1933" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akifurahia jambo na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Ernest Mangu walipokutana katika hafla ya kumuapisha IGP mpya Simon Sirro leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_1936" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro(kulia kwake) pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Dola mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kumuapisha IGP Sirro leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Waliokaa kutoka kulia IGP aliyemaliza muda wake Ernest Mangu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Makamu wa Rais Samia Suhulu Hassan,Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba.(Picha zote na: Frank Shija)[/caption] Kwa upande mwingine, IGP Sirro amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumuamini na kumteua katika cheo hicho pia amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kwa ushirikiano wake wakati alipokuwa akitumikia cheo cha Kamishna wa Polisi wa Kanda maalum ya Dar es Salaam. Kabla ya uteuzi huo, IGP Sirro alishika nyadhifa mbali mbali zikiwemo za Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamanda wa kikosi cha operesheni maalum na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam.  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi