Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Sheria ya Utakasishaji Haihusiki na Masuala ya Dhamana ya Makosa ya Kawaida - Naibu Waziri Chande
May 26, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na. Farida Ramadhan, WFM, Dodoma

Serikali imeeleza kuwa Sheria ya Kudhibiti Utakasishaji wa Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi haihusiki na utoaji dhamana kwa watuhumiwa wa makosa ya kawaida.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande alipojibu swali la Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deodatus Mwanyika, aliyetaka kujua wakati ambao Serikali itarekebisha Sheria ya Utakasishaji Fedha aliyodai inazuia dhamana kwa watuhumiwa hata kwa makosa ya kawaida.

Mhe. Chande alisema hakuna sababu ya kurekebisha Sheria hiyo kwa kuwa kifungu cha 12 cha Sheria hiyo SURA 423, kinabainisha makosa ya utakasishaji fedha haramu pekee na hakihusiki na masuala ya dhamana kwa makosa ya kawaida.

“Utaratibu wa dhamana kwa makosa mbalimbali, ikiwemo utakasishaji wa fedha haramu unasimamiwa na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, SURA 20”, alifafanua Mhe. Chande.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi