Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yawafikia 3,000 Mafunzo ya Usalama na Afya Kazini
Apr 27, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Ahmed Sagaff – DODOMA

Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan imetoa mafunzo ya usalama na afya kazini kwa watu 3,000 kupitia Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).

Akizungumza na Watanzania kupitia vyombo vya habari leo jijini Dodoma, Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako mafunzo hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi itakayoadhimishwa Aprili 28, 2022.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inasema “Kwa pamoja tushirikiane kujenga utamaduni bora wa usalama na afya mahala pa kazi”.

“Mafunzo ya usalama na afya yametolewa kwa wajasiriamali wadogo katika sekta mbalimbali wakiwemo wachimbaji wadogo, wazalishaji wa mazao ya misitu, wenye viwanda vidogo chini ya SIDO, watu wenye ulemavu na wanafunzi wa vyuo vya ufundi stadi na elimu ya juu.

“Kupitia zoezi hili, tumefanikiwa kuwafikia watu 3,000 na tunatarajia kwamba idadi hiyo itaongezeka kwani kampeni hii itaendelea hata baada ya siku ya kilele,” ameeleza Mhe. Prof.Ndalichako.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Kazi Duniani, kila mwaka takriban watu milioni mbili na laki tisa hupoteza maisha kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi