Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali yatumia Bilioni 5.6 Kuiwezesha Taasisi ya MOI kuwa na MRI,CT SCAN, X- ray na Ultra Sound
Sep 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_35873" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akipata maelezo ya hatua iliyofikiwa katika usimikaji wa mashine ya CT Scan, wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt Respicious Boniface pamoja na viongozi waandamizi wa taasisi hiyo.[/caption]

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile leo ametembelea na kukagua hali ya utoaji wa huduma katika baadhi ya  vitengo katika Taasisi ya MOI  na kukagua usimikaji wa mitambo ya kisasa katika kitengo cha radiolojia yenye thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 5.6 .

"Lengo la ziara yangu ni kukagua maendeleo ya usimikaji wa mitambo hii ya kisasa  ya MRI, CT SCAN, X-ray, Ultra sound, nimeona na kujiridhisha imekamilika kwa asilimia 99% . Naomba niwaelekeze mkamilishe mambo machache yaliyobaki ndani ya wiki hii ili wiki ijayo wagonjwa waanze kupata huduma hapa". Alisema Dkt Ndugulile.

[caption id="attachment_35872" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua moja ya machine mpya ya X-ray ya kisasa ambayo iko tayari kutumika. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface.[/caption]

viungo bandia ambapo amekagua na kujiaonea hali ya utoaji huduma na kujiridhisha kwamba huduma zimeboreka katika kipindi cha miaka 3 ya Serikali ya awamu ya tano na kwa sasa watanzania wanapata huduma kwa wakati ijapokuwa kuna changamoto chache ambazo Serikali inazishughulikia.

Aidha, Dkt Ndugulile ameupongeza uongozi wa MOI kwa kuhakikisha usimikaji wa Mitambao unafanyika kwa wakati na hali ya utoaji huduma ni nzuri na ya kuridhisha kwani wagonjwa wamekuwa wakipata changamoto ya kwenda nje ya MOI kufuata vipimo hivyo.

Akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma na usimikaji wa mitambo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amemueleza Dkt Ndugulile kwamba hali ya utoaji wa huduma ni nzuri, wagonjwa wanapata huduma stahiki kwa wakati na idadi ya wagonjwa wanaopata huduma imeongezeka maradufu baada ya eneo la kutolea huduma kuboreshwa.

[caption id="attachment_35874" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile Dkt Ndugulile akimjulia hali mtoto anayepata Huduma katika Taasisi ya MOI[/caption]

"Mhe. Naibu Waziri, hali ya utoaji huduma katika taasisi yetu ni nzuri, idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji imeongezeka na kufikia 700-900 kwa mwezi kutoka 500 kutokana ongezeko la vyumba 2 vya upasuaji katika jengo hili, awali tulikua na vyumba 6 sasa vimekuwa 8, hii nikutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali hii ya awamu ya 5 inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli" alisema Dkt Boniface

Akihitimisha yake Dkt Ndugulile amesema ni adhma ya Serikali kuhakikisha huduma zote zinapatikana hapa nchini hivyo ni vyema kama kuna kifaa chochote kinachohitajika taarifa itolewe Wizarani ili kifaa hicho kiwekwe kwenye mpango na bajeti na kununuliwa kwani utaalamu na weledi upo wakutosha.

  [caption id="attachment_35875" align="aligncenter" width="900"] Mtaalamu wa viungo bandia wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Deus David akitoa ufafanuzi kwa Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile kuhusu namna viungo bandia vinavyotengenezwa na kufanya kazi.[/caption] [caption id="attachment_35876" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na moja ya mgonjwa ambaye anatengenezewa kiungo bandia MOI ili kubainisha changamoto zilizopo zinazomkabili mgonjwa huyo.
                                                                                    (Picha zote na MOI)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi