Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yatoa Wito kwa Wakazi wa Hanang Kuhifadhi Vyanzo vya Maji
Sep 14, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Serikali imetoa wito kwa viongozi wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara kuendelea kuhamasisha wananchi kuhifadhi vyanzo vya maji ikiwemo maziwa ya Bassuto na Ziwa Eyasi.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati akijibu maswali bungeni jijini Dodoma leo Septemba 14, 2022.


Mbunge wa Hanang, Mhe. Samweli Xaday alitaka kufahamu mpango gani wa kufanya utafiti wa kujua sababu za kusambaa kwa maji ya Ziwa Bassuto na kuhama kwa samaki kwenye Ziwa Eyasi.


Mhe. Khamis alisema kwa sasa Serikali imeona hakuna haja ya kufanya utafiti wa kujua sababu ya kusambaa kwa maji na kuhama kwa samaki katika Ziwa Bassuto.

Akiendelea kujibu swali hilo, alifafanua kuwa sababu kuu ni kujaa maji wakati wa mvua nyingi, ziwa hilo ni dogo halina uwezo wa kuhifadhi maji mengi yanayosababishwa na mvua nyingi.

“Mhe. Spika maji hayo yanapojaa ziwani humo hutawanyika na kuingia kwenye Ziwa Eyasi na kwa kuwa Ziwa Bassuto lina viumbe mbalimbali ikiwemo samaki, maji hayo yanapoingia kwenye Ziwa Eyasi huingiza na viumbe mbalimbali wanaoishi kwenye Ziwa Bassuto ikiwemo samaki,” alisema.

Hivyo, Naibu Waziri Khamis alisema hali hiyo inasababisha wananchi wanaotegemea samaki wa Ziwa Basuto inawabidi kupata samaki hao kwenye Ziwa Eyasi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi