Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaelekeza Dhana ya Ukosoaji kwa Kuzingatia Misingi na Maadili
Mar 29, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_29619" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na wadau mbalimbali wa habari wakati wa mkutano ulioandaliwa na taasisi ya Twaweza kuhusiana na hali ya upatikanaji wa taarifa na dhana ya uhuru wa habari nchini. Mkutano huo ulifanyika leo.[/caption]

Serikali imesema haijazuia vyombo vya habari kukosoa utekelezaji wa sera, mikakati na programu zake na badala yake imesisitiza kuzingatia miiko na maadili ya taaluma hiyo yaliyoanishwa sheria za kimataifa.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa uzinduzi wa Awamu ya 25 ya utafiti wa sauti ya wananchi iliyotolewa na taasisi ya Twaweza.

[caption id="attachment_29613" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze akiwasilisha ripoti ya utafiti wa taasisi hiyo kuhusiana upatikanaji wa taarifa na uhuru wa habari mbele ya wadau mbalimbali wa habari. Mkutano huo ulifanyika leo.[/caption] [caption id="attachment_29614" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wadau wa habari kutoka taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa wakifuatilia mkutano ulioandaliwa na taasisi ya Twaweza kuhusiana na hali ya upatikanaji wa taarifa na dhana ya uhuru wa habari nchini. Mkutano huo ulifanyika leo.[/caption]

Dkt. Abbasi alisema kumepo na mkanganyiko mkubwa kuhusu dhana  ya uhuru wa habari, hatua inayosababisha baadhi ya vyombo vya habari kuandika na kutangaza taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikikiuka misingi ya sheria za nchi.

"Vipo baadhi ya watu wamekuwa wakifikiri dhana ya uhuru ni kusema chochote na kutumia lugha ya kejeli, hivyo ripoti hii ya utafiti tumeweza kuwa na wataalamu mbalimbali waliokuwa wakitoa mada na kujadili kwa kina misingi na miiko ya uhuru wa habari" alisema Dkt. Abbasi.

Alisema kuwa dhana ya uhuru wa habari ipo katika sheria mbalimbali za kimataifa iliyoanishwa katika misingi ya haki na wajibu, na hivyo ni wajibu wa wadau mbalimbali kuwawezesha wananchi na vyombo vya habari nchini kuweza kuelewa dhana hiyo.

[caption id="attachment_29615" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi akifuatilia mkutano uliondaliwa na taasisi ya Twaweza kuhusiana na hali ya upatikanaji wa taarifa na dhana ya uhuru wa habari nchini. Mkutano huo ulifanyika leo.[/caption] [caption id="attachment_29616" align="aligncenter" width="750"] Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe akifuatilia mkutano uliondaliwa na taasisi ya Twaweza kuhusiana na hali ya upatikanaji wa taarifa na dhana ya uhuru wa habari nchini. Mkutano huo ulifanyika leo.[/caption] [caption id="attachment_29617" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wadau wa habari kutoka taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa wakifuatilia mkutano ulioandaliwa na taasisi ya Twaweza kuhusiana na hali ya upatikanaji wa taarifa na dhana ya uhuru wa habari nchini. Mkutano huo ulifanyika leo.[/caption] [caption id="attachment_29618" align="aligncenter" width="750"] Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Vicensia Shule akizungumza na wadau mbalimbali wa habari wakati wa mkutano ulioandaliwa na taasisi ya Twaweza kuhusiana na hali ya upatikanaji wa taarifa na dhana ya uhuru wa habari nchini. Mkutano huo ulifanyika leo. (Na: Mpiga Picha Wetu)[/caption]

Alioongeza kuwa Serikali imeendelea kuongeza wigo mpana wa uanzishaji wa vyombo vya habari nchini ikiwemo kutoa idadi kubwa ya leseni za uanzishaji wa vituo vya redio hususani katika maeneo ya vijijini, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kuweza kupata taarifa mbalimbali za umma.

Kuhusu taarifa ya utafiti huo, Dkt. Abbasi alisema Serikali itatumia taarifa ya ripoti ya utafiti huo kupata mrejesho na kuainisha maeneo yote ili kuchambua hoja na kuweza kuangalia maeneo yenye changamoto ili kuweza kuboresha mfumo wa utoaji na upatikanaji wa taarifa za Serikali kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema Serikali tayari imetoa maelekezo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi zote za umma nchini kuweka utaratibu wa kutoa taarifa zake kwa umma kwa kuwa suala la utoaji wa taarifa si utashi na badala yake ni utekelezaji wa matakwa ya sheria.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze alisema katika utafiti huo uliohusisha jumla ya watu 1500, ulionyesha kuwa wananchi wana imani na taarifa na imani zinazotolewa na Viongozi Wakuu wa Serikali ikiwemo Rais ikifuatiwa na Waziri Mkuu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi