[caption id="attachment_16055" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakisaini Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.[/caption]
Na. Neema Mathias- MAELEZO.
Serikali imeendelea kutekeleza ahadi ya ujenzi wa reli mpya ya kisasa (Standard Gauge) kutoka Dar es Salaam mpaka Kigoma baaada ya leo kusaini mkataba na kampuni ya Yapi Markezi ya Uturuki kujenga sehemu ya pili ya reli hiyo kutoka Morogoro mpaka Makutupora, Dodoma.
Mkataba huo umesainiwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Yapi Markezi, Mr.Erdem Arioglu.
Kabla ya kusaini mkataba, Kadogosa alieleza kuwa mkataba huo wa ujenzi wa reli yenye urefu wa kilometa 336 kutoka Morogoro mpaka Makutupora-Dodoma, unahusisha ujenzi wa kilometa 86 za njia ya kupishania treni na maeneo ya kupangia mabehewa 422 kwa uzani wa tani 35 kwa wekeli.
[caption id="attachment_16056" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakibadilishana Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.[/caption]Pia ujenzi wa miundombinu ya umeme wa kuendeshea treni, ujenzi wa madaraja Zaidi ya 223, makaravati Zaidi ya 143, tanuru la kupitishia njia ya reli lenye urefu wa kilometa 2.5, stesheni nane za abira na njia za kupishania treni zenye urefu wa kilometa mbili.
“Kutokana na uwezo wa reli hii kusafiri kwa mwendo wa kkilometa 160 kwa saa, kutajengwa ukuta pande zote mbili za reli kuanzia Morogoro mpaka Makutupora, Dodoma ili kuhakikisha usalama wa watu na wanyama,” alieleza Kadogosa
[caption id="attachment_16057" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakionyesha kwa waandishi wa habari Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma).[/caption]Pamoja na kujenga ukuta pembezoni mwa reli, Kaimu Mtendaji Mkuu huyo alisema kuwa kutajengwa vivuko kwa ajili ya waenda kwa miguu pamoja na wanyama ambao watakaokuwa wanatoka upande mmoja wa reli kwenda upande mwingine.
Kwa upande wake Waziri Ujenzi, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano imeupa kipaumbele mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ikiwa ni sehemu ya kuimarisha miundombinu ya usafirishaji nchini ili kuinua uchumi wa Tanzania.
“Kukamilika kwa ujenzi huo kutatoa fursa kwa viwanda na wafanyabiashara kufanya chaguo la njia gani ya usafiri wenye tija watumike kusafirisha bidhaa zao. Njia hii ya reli itapunguza la gharama za usafirishaji na kuondoa hofu ya kusafirisha mizigo kwa muda mrefu kwani reli hii ya kiasasa ina uwezo wa kubeba mizigo mikubwa na inayokwenda umbali mrefu na kwa kasi kubwa,” alifafanua Prof. Mbarawa.
[caption id="attachment_16064" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma).[/caption]Aidha alisema kuwa serikali kupitia bajeti ya mwaka 2016/2017 ilitenga kiasi cha shulingi trilioni moja na katika bajeti ya mwaka 2017/2018 imetenga shilling bilioni 900 kwamba Serikali inaendelea kutafuta vyanzo vya fedha kuwa kutafuta mikopo ya bei nafuu na inaitaka serikali hiyo kukamilisha ujenzi huo chini ya miezi 36.
[caption id="attachment_16058" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho akizungumza akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.[/caption]Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki Bw. Erdem Arioglu ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa hatua ya ujenzi wa reli hiyo na amesema kuwa mradi huu utazidi kuimarisha uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Uturuki na kuishukuru RAHCO kwa kuwaamini na kuwapa kuwapa kazi ya ujenzi wa reli hiyo.
Awamu ya pili ya utiaji saini ujenzi wa reli mpya ya standard gauje yenye uwezo wa kusafirisha mizigo tani million 17 kwa mwaka ni mwendelezo wa ujenzi wa awamu ya kwanza uliozinduliwa Aprili 12 wa Dar es Salaam- Morogoro wenye jumla ya kilomita 205, ikiwa ni miaka 112 ytangu reli ya zamani ijengwe.
[caption id="attachment_16059" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.[/caption] [caption id="attachment_16060" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hawa Ghasia akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.[/caption] [caption id="attachment_16061" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Wahandisi kutoka kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakifuatilia hafla ya utiaji saini saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.[/caption] [caption id="attachment_16062" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Wafanyakazi kutoka shirika la Reli Nchini (TRL) na kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) wakifuatilia hafla ya utiaji saini saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.[/caption] [caption id="attachment_16063" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki, Erdem Ariogl pamoja na Kaimu Balozi wa nchini hiyo Yunus Belet wakati wa utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma).[/caption]