Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yatekeleza Miradi 1,498 ya Maji Nchini
Jul 25, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33861" align="aligncenter" width="800"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Wanahabari leo Mjini Dodoma[/caption]

Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imetekeleza jumla ya miradi 1,493 ya maji vijijini kufikia Desemba, 2017 na ujenzi wa miradi 366 unaendelea kutekelezwa sehemu mbalimbali nchini.

Hayo yameelezwa leo, Jijini Dodoma na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa ahadi za Serikali.

"Mwaka 2017, Serikali iliendelea kutekeleza miradi ya maji vijijini kupitia programu ya kuendeleza sekta ya maji kwa lengo la kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji vijijini," amesema Dkt. Abbasi.

[caption id="attachment_33860" align="aligncenter" width="800"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Wanahabari leo Mjini Dodoma[/caption]

Aidha, amesema Serikali imetimiza ndoto ya kuendelea kulifufua Shirika la Ndege kwa kulera Boeing 787 Dreamliner na ndege nyingine mbili za C Series zinatarajiwa kufika Novemba mwaka huu wakati Boeing nyingine moja inatarajia kuwasili 2020.

"Manufaa ya ndege hizi yameanza kuonekana ambapo zinasaidia wananchi wengi kusafiri kwa haraka na kufanya biashara zao kwa haraka. Tangu tulete ndege hizi abiria wa ATCL wameongezeka kufikia 107,207 katika mwaka 2016/2017 kutoka 49,173 mwaka 2015/2016 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 118," alifafanua Dkt. Abbasi.

Vile vile amesema katika Mwaka wa Fedha 2017/2018, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 15.5 kuanzia Julai 2017 hadi Juni, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 14.4 ambazo zilikusanywa katika kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017, kiasi hiki ni sawa na ukuaji wa asilimia 7.5.

Dkt. Abbasi amesema, kutokana na utendaji makini wa Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano kwa ujumla hata mashirika ambayo yalikuwa hayatoi gawio kwa Serikali sasa yanatoa.

"Juzi mmesikia zaidi ya shilingi bilioni 700 zimekusanywa kama gawio na mgawo wa asilimia 15 kutoka taasisi na mashirika ya umma na binafsi 43 na taarifa za sasa ni kuwa fedha hizi zitaongezeka hadi zaidi ya bilioni 800 ikiwa ni baada ya taasisi nyingine kuhamasika na hii ni ongezeko la asilimia zaidi ya 500," amefafanua Dkt. Abbasi.

Amesema kuwa, katika kutekeleza agizo la kuhamia Dodoma tayari watumishi 6,400 wamehamia mkoani humo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi