Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yatatua Tatizo la Ununuzi wa Pamba
Jul 15, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_45295" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba, Julai 15, 2019. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.[/caption]

*Waziri Mkuu asema hadi Julai 30 pamba yote itakuwa imenunuliwa 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia tarehe 30 mwezi Julai pamba yote iliyoko katika mikoa mbalimbali nchini inayolima zao hilo itakuwa imeshanunuliwa na wakulima wote kulipwa fedha zao.

Kauli hiyo imetolewa leo (Jumatatu, Julai 15, 2019) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Mbutu na Mwabakima wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Amesema Serikali imeamua kuingilia kati suala la ununuzi wa zao la pamba kutokana na kusuasua kwa soko lake kwa kutoa dhamana ili kuwawezesha wanunuzi kukopeshwa fedha na benki mbalimbali kwa ajili ya kununulia pamba kutoka kwa wakulima.

[caption id="attachment_45293" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kasism Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Katibu na Meneja wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga kuhusu pamba iliyokusanywa na wakulima kwenye ghala la ushirika huo, Julai 15, 2019.[/caption] [caption id="attachment_45292" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha Ushirika kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo, Julai 15, 2019.[/caption]

Hivyo, amewataka wakuu wa mikoa na wilaya katika maeneo yote yanayolima zao hilo wawasimamie ipasavyo wanunuzi wote ili kuhakikisha fedha zitakazopatikana zinakwenda kutumika kwa ajili ya kununulia pamba na si vinginevyo, ambapo kibali cha dhamana kinatarajia kutoka leo.

Amesema kumekuwa na kusuasua kwa ununuzi wa zao hilo tangu kuanza kwa msimu wa mwaka huu jambo ambalo Serikali haiwezi kulifumbia macho suala hilo, hivyo jana alikutana na kufanya mazungumzo na wadau wa zao hilo wakiwemo wanunuzi na wamekubaliana kununua pamba yote.

“Tunatambua adha mliyoipata tangu kuanza kwa msimu wa mwaka huu na hayo ni mapito tu. Nawasihi muwe na amani kwani Serikali yenu inafuatilia suala hili na Rais Dkt. John Magufuli anataka kuona pamba yote inatoka kwa wakulima ili kuwawezesha kupata tija.”

[caption id="attachment_45294" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mikokoteni iliyosheheni pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga alikofanya ziara ya siku moja ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo, Julai 15, 2019. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.[/caption]

Kadhalika, Waziri Mkuu amewasihi wakulima wa zao hilo la pamba na wakulima wa mazao mengine nchini wahakikishe mara baada ya kuuza mazao yao wanatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kununulia pembejeo watakazozitumia katika msimu ujao.

Awali, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga alisema Serikali itahakikisha inaendelea kutafuta masoko ya mazao hayo ndani na nje ya nchi ili kuwawezesha wakulima kuwa na uhakika wa masoko kwa mazao yao na hivyo kujiongezea tija.

Pia, Waziri huyo amesema mbali na kutafuta masoko, Serikali imedhamiria kufufua viwanda mbalimbali vya nguo hapa nchini ili kuwawezesha wakulima wa zao la pamba kuwa na soko la uhakika. “Kuhusu suala la maghala tunatambua tatizo hilo na tutahakikisha tunayaboresha ili pamba iweze kuhifadhiwa katika mazingira bora”.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATATU, JULAI 15, 2019.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi