Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yatangaza Fursa za Ajira 500 kwa Madereva Pikipiki Nchini UAE
Dec 29, 2025
Na Baraka Messa – MAELEZO

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi na Mahusiano, imetangaza nafasi 500 za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye uzoefu katika fani ya udereva wa pikipiki, kwenda kufanya kazi Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Target Tours and Labour Supply Company Limited kutoka nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu ( UAE) imeeleza kuwa  ajira  hizo zimetolewa na Kampuni ya Velogistic Delivery Service LLC ya UAE.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa  waombaji wote  wanapaswa kuwa na umri  kuanzia miaka 20 hadi 37,  elimu ya msingi au sekondari, leseni halali ya udereva wa pikipiki, uzoefu wa angalau miaka miwili katika udereva wa pikipiki, hati ya kusafiria na uwezo wa kuzungumza na kuandika lugha ya Kiingereza.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa nafasi hizo zimetengwa kwa waombaji wa kiume pekee huku zoezi la usaili likitarajiwa kuanza  Januari 19 hadi 21, 2026 jijini Dar es Salaam, kisha kuendelea katika Mikoa ya  Mwanza kuanzia Januari 22 hadi 24, Tanga kuanzia Januari 26 hadi 28, 2026.

Serikali inatoa wito kwa vijana wenye sifa kote nchini kuchangamkia fursa hiyo kama sehemu ya mkakati wa kupanua ajira kwa Watanzania kupitia ushirikiano wa kikanda na kimataifa.  

Aidha, waombaji wote wanatakiwa kutuma wasifu (CV) zao kupitia anuani ya info@targettours.co.tz au kupiga simu 
namba +255784989905,
+255766712222,

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi