Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yatangaza Ajira Mpya 12000
Nov 14, 2025
Serikali Yatangaza Ajira Mpya 12000
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wabunge pamoja na viongozi mbalimbali kabla ya kufungua rasmi Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa Bunge Jjjini Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.
Na Mwandishi Wetu - Dodoma.

Serikali imeanza kutekeleza ahadi zake za muhula mpya ndani ya siku 12 tangu kuanza kwa awamu ya pili ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwemo kutangaza jumla ya ajira 12,000 katika sekta za afya na elimu ili kujibu mahitaji ya wananchi Kwa kuboresha huduma hizo hapa nchini.

Akifungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Rais Samia amesema safari kubwa ya kutembelea maeneo mbalimbali nchini imesaidia kukusanya maoni na changamoto za wananchi ambazo serikali imejielekeza kuzifanyia kazi kwa kauli mbiu ya kazi na utu.

" Tayari tumeshatangaza nafasi za ajira 7,000 za walimu na nafasi za ajira 5,000 za watumishi wa afya. Hatua hii ni mwanzo kujibu kiu ya wananchi ya kuboresha huduma za afya na elimu nchini" amesema Rais Samia.

Ameongeza kuwa jitihada zote za maendeleo zinazochukuliwa na Serikali zitakuwa zinalenga kuinua utu na thamani ya Mtanzania, huku serikali ikizingatia mageuzi ya sera na mifumo ili kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Rais Samia amesema kipaumbele cha kwanza ndani ya siku 100 za mwanzo ni utumishi na utawala bora, akibainisha kuwa serikali inaendelea kubadilisha mifumo na kuimarisha uwajibikaji.

Amewataka mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, na maafisa tarafa kuwa karibu zaidi na wananchi ili kufahamu changamoto zao na kusimamia utekelezaji wa mipango ya serikali kwa kasi zaidi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi