Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yarahisisha Ukusanyaji wa Takwimu za Vifo Vinavyotokea Katika Ngazi ya Jamii Nchini
Oct 31, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37649" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na baadhi ya Wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na Maafisa Afya mkoani Iringa wakati wa kukabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo ngazi ya jamii kwa Maafisa Afya mkoani humo.[/caption]

Na: WAMJW-Iringa

SERIKALI kupitia Wizara ya afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imerahisisha ukusanyaji wa takwimu za vifo vinavyotokea kwenye ngazi ya jamii nchini kwa kugawa vifaa maalumu vya kukusanyia takwimu hizo kwa Maafisa afya katika kata za mkoa wa Iringa.

Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki  Ulisubisya wakati akikabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu hizo  kwa Maafisa Afya leo  Mkoani Iringa.

“Takwimu zitakazokusanywa kuhusu vifo na  Maafisa hawa wa afya  kutokana na Mifumo hii zitawasaidia madaktari kujadili changamoto pamoja na sababu za vifo hivyo ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo na kuweza kupunguza idadi ya vifo nchini” alisema Dkt. Ulisubisya.

[caption id="attachment_37651" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya katikati akionesha Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo ngazi ya jamii pamoja na Maafisa afya wa kata mbalimbali Mkoani Iringa.[/caption] [caption id="attachment_37652" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa iringa Bw. Fikira Kissimba akiongea nna na baadhi ya Wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na Maafisa Afya mkoani Iringa wakati wa kukabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo ngazi ya jamii kwa Maafisa Afya mkoani humo.[/caption]

Aidha,Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa takwimu hizo zikikusanywa kikamilifu zitasaidia kutoa elimu kwa jamii na kupunguza imani za kishirikina kwa wananchi kwani zitaleta picha sahihi ya kugundua vyanzo vya  vifo hivyo kwenye jamii husika.

Hata hivyo Dkt.  Ulisubisya amewataka maafisa hao kutumia vifaa hivyo kwa matumizi ya kazi ya kukusanyia takwimu na sio matumizi binafsi na kama itatokea afisa afya yeyote atakayehama kituo cha kazi  basi arudishe  ofisini kwa ajili ya mtumishi mwingine atakayekuja.

Kawa upande wake Kaimu katibu Tawala wa Mkoa iringa Bw. Fikira Kissimba amesema kuwa mfumo huo wa ukusanyaji taarifa zitasaidia pia uandikishwaji wa mirathi ya marehemu wakati ndugu husika anapokwenda kufungua mirathi yake mahakamani.

[caption id="attachment_37653" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisyakushoto akimkabidhi Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Mji bw. Fredrick Kayombo kulia wakati wa kukabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo ngazi ya jamii kwa Maafisa Afya mkoani humo.[/caption] [caption id="attachment_37654" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathimini kutoa Wizara ya Afya Bw. Tumainieli Macha wa kwanza kulia akifuatilia kwa makini maelekezo ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa kukabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo ngazi ya jamii kwa Maafisa Afya mkoani Iringa.(Picha na Wizara ya Afya)[/caption]

Naye Mratibu wa usajili wa Takwimu wa Masula muhimu ya Binadamu nchini Dkt. Gregory Kabadi amesema kuwa jumla ya Kompyuta kibao (Tablets) zilizogawiwa ni 106 kwa kila kata ya mkoani Iringa na thamani yake ni takribani shilingi Milioni 61.5.

Aidha , Dkt Kabadi amesema kuwa zoezi hilo limeanza kwa majaribio katika halmashauri tano kwenye mikoa mitatu ikiwemo Pwani,Tanga na Morogoro na kufanya tathimini ya utekelezaji wa mifumo hiyo katika mkoa wa Iringa kabla ya kutumika nchi nzima.

Kwa upande  wake Afisa afya wa kata ya Kitwilu Bw. Wilson Ntagondwa amesema kuwa kupitia mfumo huo waliokabidhiwa itawasaidia kukusanya takwimu kwa urahisi hivyo kupelekea kujua sababu zinazosababisha vifo na kusaidia kupanga maendeleo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi