Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yalenga Kuimarisha Usawa Mapambano Virusi vya UKIMWI
Nov 30, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene amepongeza Tume ya Kudhibiti UKIMWI, Wizara ya Afya na Wizara ya TAMISEMI katika Mkakati wa kupambana na UKIMWI kama janga la kitaifa.

Hayo yamesemwa na Waziri na Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene Jijini Dar es saalam, wakati wa uzinduzi wa taarifa ya hali ya UKIMWI duniani yenye Kauli Mbiu inayosema "Dangerous Inequalities" iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Ukimwi Duniani UNAIDS, Bi. Winnie Byanyima.

“Serikali imedhamiria kuweka usawa wa kijiografia, kimazingira, usawa kati ya watoto na wakubwa na usawa wa kiuchumi ili kuhakikisha watu wote wanapata huduma sawa ili wasiathirike na wale walioathirika wapate huduma za matibabu lakini pia huduma sawasawa kuhakikisha wanaendesha maisha yao.”

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia UKIMWI Duniani UNAIDS, Bi. Winnie Byanyima amesema Tanzania imejitahidi kupunguza ongezeko la maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kila mwaka kwa miaka kumi mfululizo.

“Tanzania imejitahidi kupunguza vifo vinavyosababishwa na UKIMWI na imekuwa ikifanya vizuri katika mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI.”

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi