Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yajipanga Kurekebisha Mifumo ya Kidijitali Kuongeza Ufanisi
Dec 12, 2025
Serikali Yajipanga Kurekebisha Mifumo ya Kidijitali Kuongeza Ufanisi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Mhe. Ridhiwani Kikwete akieleza kwa Waandishi wa Habari mikakati ya Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kipindi cha miaka mitano ijayo leo Desemba 12 , 2025 jijiji Dar es Salaam.
Na Bupe Mwaiseje -MAELEZO 

 Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali imefanya marekebisho kwenye mifumo ya Kidijitali ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma .

 Ameyasema hayo leo Desemba, 12, 2025 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari na kusema kuwa serikali inataka iondoke kwenye mfumo wa makaratasi.

 Ameeleza kuwa Chama Tawala kupitia Ilani yake ibara ya 49, ibara ndogo ya 3 kimeelekeza Serikali kuimarisha mifumo ya kiufanisi na uwajibikaji katika utumishi wa umma. Waziri Kikwete amesema Ofisi ya Rais Manajementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imefanya marekebisho ya mifumo ikiwemo mifumo ya E- Mrejesho ambayo itawawezesha wananchi hususani walio mbali na maeneo ya ofisi kutoa maoni, malalamiko na pongezi kuhusu huduma zinazotolewa na Serikali na taasisi zake. 

"Mfumo huu unapatikana kupitia simu ya mkononi kwa kupiga * 152*00# kisha mwananchi kuchagua namba 9 kisha 2 na kumalizia namba 2, mfumo huu kwa sasa utakuwa na moduli ya sema na kiongozi  ambayo wananchi wote wataweza kutoa mrejesho kwa kuwasilisha taarifa, pongezi, malalamiko na maoni", amesema Mhe. Waziri.  

Aidha, amesema taarifa hizo zitasaidia kutambua maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi na marekebisho kwa haraka, sambamba na kuanzishwa kwa programu ambayo itawawezesha wananchi kutoa mrejesho wa haraka na uwazi ili kuimarisha uwajibikaji na majibu kwa Serikali. 

Amewahakikishia wananchi na viongozi wa umma kuwa mfumo huo utafanya kazi kwa ufanisi hivyo kuwataka kuutumia ili kuongeza ufanisi wa kazi na uwajibikaji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi