Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yahamasisha Matumizi ya Gesi Majumbani
May 10, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Frank Mvungi-Maelezo

Serikali Kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imeanza matarayarisho ya kutekeleza mradi wa kuunganisha gesi majumbani ambapo awamu ya kwanza ya mradi huo umepita  katika eneo la Mikocheni  Jijini  Dar es Salaam.

Akijibu swali la mheshimiwa Zainab Mndolwa Amiri aliyetaka kujua  ni lini Serikali itapunguza bei ya gesi kwa matumizi ya nyumbani kuwawezesha wananchi wengi zaidi kutumia gesi kwa matumizi yao ya Nyumbani, Naibu  Waziri wa Nishati  Mhe. Subira Mgalu amesema kuwa Serikali imeendelea kuhamasisha wawekezaji katika sekta ya gesi kwa matumizi ya majumbani.

Mradi wa kusambaza gesi hiyo utaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini lengo likiwa kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma hiyo ili kuchochea maendeleo.

“Mpaka sasa Makampuni mengi yameanza kujenga miundo mbinu ya gesi katika sehemu mbalimbali za nchi na kuonesha nia ya kushirikiana na Serikali katika kusambaza gesi asilia nchini” Alisistiza Mhe. Mgalu

Akifafanua Mhe. Mgalu amesema kuwa kwa hivi sasa gesi inayotumiwa na wananchi kupikia majumbani ni liqudified Petroleum gas ( LPG) ambayo huagizwa na wafanyabiashara kutoka kama ilivyo katika mafuta ya petroli, dizeli,  mafuta ya taa na ndege. Aidha gesi hii hujazwa katika mitungi kwa ujazo tofauti.

Aliongeza kuwa mradi wa majaribio wa gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya nyumbani ulianza kupitia mradi wa mfano (pilot project) ambapo nyumba 70 zilizoko Mikocheni Jijini Dar es Salaam zimeunganishwa na gesi kwa matumizi ya nyumbani.

Gesi iliyogunduliwa hapa nchini ni Gesi Asilia (Natural Gas) ambayo husafirishwa kutoka kwenye visisima vya gesi hadi kwa watumiaji kupitia mabomba mpaka kwa watumiaji wakubwa wa gesi hapa nchini ni viwanda na mitambo ya kufua umeme.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi