Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaanza Rasmi Kutoa Leseni za Machapisho Yote Nchini
Aug 23, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_9971" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu kuanza kwa utoaji wa leseni za machapisho leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Habari na Picha Bw. Rodney Thadeus.[/caption]

Na. Bushiri Matenda - MAELEZO

Serikali imeanza rasmi kutoa leseni za uchapishaji wa magazeti, majarida na machapisho mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sheria mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi ametangaza kuanza rasmi kwa utoaji wa leseni leo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na vyomba vya Habari.

Ameeleza kuwa utoaji wa leseni hizo ni utekelezaji wa matakwa ya kifungu cha 5(e) cha sheria ya Huduma za Habari, 2016 inayotaka magazeti na majarida yote nchinini kusajiliwa na kupata leseni za uendeshaji.

[caption id="attachment_9973" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kuanza kwa utoaji wa leseni za machapisho, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Usajili Bw. Patrick Kipangula na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Habari na Picha Bw. Rodney Thadeus.[/caption] [caption id="attachment_9974" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Usajili Bw. Patrick Kipangula (kushoto) akisoma baadhi ya masharti ya kanuni za usajili wa machapisho kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Habari na Picha Bw. Rodney Thadeus.[/caption]

“Chapisho lolote litakalotolewa katika chombo cha habari bila kuwa na leseni ni kosa la jinai kisheria hivyo pia waombaji wapya wanaruhusiwa kujisajili na kupewa leseni” Dkt. Abbasi.

Ameeleza kuwa utaratibu wa sasa unafuta mfumo wa awali wa utoaji wa Hati za Usajili wa magazeti na majarida uliokuwa ukitumika kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo kwa sasa imefutwa rasmi, hivyo leseni hizo zitahuishwa kila mwaka kwa mujibu wa kanuni namba 8 (3) na 12 (1) (2) za sheria za Huduma za Habari za 2017.

[caption id="attachment_9976" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu kuanza kwa utoaji wa leseni za machapisho.[/caption] [caption id="attachment_9977" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya kuanza kwa utoaji wa leseni za machapisho.[/caption]

Picha na Idara ya Habari  (MAELEZO)

Dkt. Abbasi anasema kwamba lengo la usajili huu ni kuifanya tasnia ya habari nchini kuwa taaluma inayotambulika na kuheshimika kuliko ilivyo sasa.

Zoezi hilo la utoaji leseni za magazeti, majarida na machapisho mbalimbali ya Umma na binafsi linafanyika katika Ofisi zake za Idara ya Habari – MAELEZO Dar es salaam na Dodoma ambapo fomu za leseni zinapatikana katika tovuti rasmi ya Idara ambayo ni www.maelezo.go.tz

Idara ya Habari (MAELEZO) ambayo ndio mratibu Mkuu wa zoezi hilo la utoaji leseni kwa Magazeti, Majarida na Machapisho mbalimbali ya umma na watu binafsi linaendesha zoezi hilo kuanzia leo mpaka Oktoba 15, 2017 kwa wamiliki wa Magazeti na Majarida ambao wana usajili wa zamani, ukomo huo hautawahusu wasajiliwa wapya.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi