[caption id="attachment_7607" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na watumishi wa Radio ya Efm (hawapo katika picha) alipofanya ziara ya kutembelea chombo hicho cha habari leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]
Na Lorietha Laurence.
Serikali imeeleza kuwa inathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Vyombo vya Habari nchini katika kuhakikisha kuwa jamii inapata taarifa sahihi na kwa wakati.
Akizungumza katika ziari yake alipotembelea vyombo vya habari vya Radio EFM na Radio One/ ITV leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kuwa lengo kubwa la Serikali ni kuwepo kwa ushirikiano mzuri na sekta ya habari nchini.
“Lengo la ziara hii ni kuimarisha uhusiano baina ya Serikali na vyombo vya habari pamoja na kufahamu utendaji wenu wa kazi na namna mnavyosimamia maudhui ya vipindi vyenu mnavyoviandaa” amesema Prof. Gabriel
[caption id="attachment_7611" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Radio ya Efm Bw. Francis Ciza wakati wa ziara yake kutembelea chombo hicho cha habari leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]Aidha aliongeza kuwa ni jambo jema linalofanywa na watanzania wazawa kuwekeza katika sekta ya habari kwa kuwa dunia ya sasa imetawaliwa na utandawazi kupitia taarifa mbalimbali zinazotolewa zenye lengo la kuhabarisha na kujenga taifa letu.
Kwa upande mwingine Prof. Gabriel amewataka watumishi wa vyombo hivyo vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na uzalendo ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Pia amewataka watumishi wa vyombo hivyo vya habari kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa kujituma ili kupata matokeo chanya katika soko la ushindani na kuifikia jamii kubwa zaidi katika kutoa habari za uhakikia na zenye usahihi.
[caption id="attachment_7608" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Radio ya Efm pamoja na watendaji wa Wizara ya Habari wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_7610" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa ITV/Capital Tv Bw. Koigi Wacharia wakati wa ziara yake kutembelea Chombo hicho cha Habari leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]Sambamba na hilo Prof. Gabriel amevitaka vyombo hivyo vya habari kuzingatia maudhui yanayoendana na jamii ya kitanzania pale wanapoandaa vipindi mbalimbali ili kujenga jamii yenye utamaduni mzuri ikiwemo kufanya kazi kimkakati.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Redio Efm, Bw. Denis Ssebo amesema kuwa uongozi wa radio yake upo tayari kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali lengo likiwa ni kuhakikisha wanafuata sheria na kanuni za utangazaji ili kufanya kazi kwa kiwango chenye ubora .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Radio One/ITV Bibi. Joyce Mhaville ameishukuru serikali kupitia wizara ya Habari kwa kuonyesha ushirikiano mzuri na vyombo vya habari ikiwemo kufanya kazi kwa karibu na kuviwezesha vyombo hivyo kupata habari zenye ukweli na uhakika.