Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaagiza Udhibiti kwenye Maeneo yenye Rekodi za Rushwa
Dec 11, 2025
Na Bupe Mwaiseje - MAELEZO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameongoza mkutano wa maadili kwa viongozi wa Umma na kubainisha maeneo yanayohitaji hatua za haraka kwenye maeneo yenye rekodi za rushwa.

Ameyasema  hayo leo, Desemba 11, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi na watendaji wa Sekretariati ya Maadili katika Ofisi za Tume ya Maadili jijini Dodoma.


"Maadili na Matamko yawe kwa kila mtumishi wa umma na kipaumbele kiwekwe kwenye maeneo ambayo yanavivutio vingi vya rushwa", amesema Mhe. Waziri Mkuu


Amesema kuwa, eneo la manunuzi lina mapungufu mengi, ikiwemo hati zisizowalazimisha watu wa manunuzi kuweka wazi mali na madeni yao, suala linalohitaji kutizamwa upya ili kuondoa mianya ya rushwa.

" Yapo maeneo ambayo fedha ya umma inaweza kupotea na Watanzania wanaweza wasijue lakini yana madhara makubwa. " Amesema Mhe. Mwigulu.

Aidha, ameiagiza Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma kuanzisha kitengo cha siri  cha uchunguzi wa mwenendo wa viongozi na watumishi wa umma kwa kufanya marekebisho ya sheria na kanuni zinaonekana kuchochea vitendo vya rushwa.

Hata hivyo ameagiza kuwepo kwa wasimamizi masuhuli na kamati za zabuni ili kuongeza nguvu ya kukomesha jambo la rushwa nchini.
 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi