Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kusimamia Maslahi ya Watanzania Ujenzi Bomba la Mafuta
Jan 22, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_27643" align="aligncenter" width="750"] Kamishna Msaidizi wa Mafuta toka Wizara ya Nishati Bibi. Mwanaamani Kidaya akimwelekeza jambo Mratibu wa Mradi wa Bomba la Mafuta toka Hoima , Uganda hadi Chongoleani Tanga, Tanzania Bw. Salum Mnuna wakati wa mkutano wa wadau wa Mafuta toka sehemu mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema itasimamia maslahi ya Wajasiriamali na makampuni ya Kitanzania yatayokidhi viwango vya kimataifa katika utoaji wa huduma ili kuwaweka kunufaika na fursa ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kaabale nchini Uganda hadi ghuba ya Chongoleani Tanzania.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kamishina Msaidizi wa Mafuta wa Wizara ya Nishati, Mwanaamani Kidaya katika warsha iliyoshirikisha Wadau kutoka sekta binafsi na makampuni mbalimbali ya kimataifa kujadili ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.

[caption id="attachment_27644" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa Kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa Mafuta, Gulf Interstate Engineering akiwasilisha mada kuhusu fursa na vigezo vitakavyotumika kutoa ajira wakati wa ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta toka Hoima , Uganda hadi Chongoleani Tanga, Tanzania wakati wa mkutano wa wadau wa Mafuta toka sehemu mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_27645" align="aligncenter" width="750"] Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATGOS), Abdulsamad Abdulrahim akielezea namna ambavyo wazawa wanaweza kunufaika na ujenzi wa Bomba la Mafuta toka Hoima , Uganda hadi Chongoleani Tanga, Tanzania wakati wa mkutano wa wadau wa Mafuta toka sehemu mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Bi. Mwanaamani alisema ujenzi wa bombahilo ni fursa ya kipekee ambayo haina budi kutumiwa kikamilifu kwa ajili ya kuinua uchumi wa Tanzania na ni wajibu wa makampuni na wajasiriamali kuhakikisha kuwa wanatimiza viwango vikihitajika na kampuni za ukandarasi zitakazokuwa zikisimamia ujenzi huo.

“Mradi huu unatarajia kupita katika mikoa 8 ya Tanzania ambapo kati ya kilometa 1445 za bomba hilo, kilometa 1147 zipo Tanzania, hivyo ni wajibu wa makampuni yetu kuhakikisha kuwa yanakidhi viwango vya kimaitafa vinavyowekwa na makampuni ya ukandarasi na Serikali itawasimamia” alisema Mwanaamini.

Aidha Mwanaamini alisema mradi huo wa bomba la mafuta unatarajia kutekelezwa katika viwango vya kimataifa, ambapo huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinatarajia kuwanufaisha wananchi wa Tanzania na Uganda, hivyo makampuni ya Kitanzania hayana budi kuhakikisha kuwa yanatoa huduma bora na za viwango vya juu.

[caption id="attachment_27648" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wadau kutoka sekta binafsi na makampuni mbalimbali ya kimataifa kujadili ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania. (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa  Chama cha Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATGOS), Abdulsamad Abdulrahim alisema warsha hiyo imeshirikisha watalaamu kutoka Mataifa mbalimbali duniani ili kuwawezesha Watanzania kuelewa viwango vya kimataifa vinavyotumika kwa ajili ya kujenga miradi mbalimbali ikiwemo bomba la mafuta.

Aliongeza kuwa kongamano hilo pia limelenga kujenga uwezo na fursa makampuni na wajasiriamali Watanzania kupata uelewa kuhusu utekelezaji wa mradi wa bomba la gesi pamoja na fursa mbalimbali wanazopaswa kuzitumia ili ziweze kuwainua kiuchumi.

“Makampuni kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Uingereza, Kuwait, Dubai, India, Malaysia, Argentina na Marekani yameshiriki katika mkutano huu, hivyo ni wajibu wa Watanzania kuchangamkia fursa hiyo katika bomba la mafuta ambalo litaweza kuzalisha ajira kwa wananchi wengi zaidi” alisema Abdulrahim.

Abdulrahim alisema kuwa kwa sasa ujenzi wa bomba hilo umefikia katika hatua nzuri ya utekelezaji wake, na kuwataka Watanzania kuwa tayari wakati mchakato wa kutafuta kampuni mbalimbali za ukandarasi utakapoanza kutangazwa na Serikali.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye alisema mradi wa ujenzi wa bomba hilo unatarajia kuzalisha ajira nyingi kwa Watanzania, hivyo ni wajibu wa makampuni ya Kitanzania kuhakikisha kuwa yanafanya kazi kwa kuzingatia viwango na maadili ya kimataifa.

Aliongeza kuwa TPSF itahakikisha kuwa inaisaidia Serikali katika kutoa taarifa za mapema kwa Watanzania kupitia zabuni zitakazotangazwa na makampuni mbalimbali pindi mchakato wa ujenzi wa bomba hilo utakapoanza.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi