Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuongeza Pato la Taifa kwa Kubuni Vyanzo Vingine vya Mapato
Jun 08, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na: Jonas Kamaleki

Serikali imebuni vyanzo vingine vya mapato ili kupanua wigo wa kodi kwa ajili ya maendeleo endelevu nchini na kukuza uchumi wa Taifa.

Dkt. Mpango alisema kuwa Serikali ikusudia kuongeza mapato kwa kuwatambua wafanyabiashara wasio rasmi kwa kuwapatia vitambulisho maalum kulingana na biashara zao.

“Serikali itawatambua rasmi wafanyabiashara wadogo wadogo wasio rasmi na wanaofanyia biashara katika maeneo yasiyo rasmi mfano mama lishe, wauzaji mitumba wadogowadogo, wauzaji wa mazao ya kilimo wadogo kama mboga mboga, ndizi, matunda, na kadhalika kwa kuwapatia vitambulisho maalum vya kazi wanazozifanya”, alisema Dkt. Mpango.

Aidha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa Serikali itaendelea na ukusanyaji wa kodi ya majengo (yaliyothaminiwa na yasiyothaminiwa) kwenye halmashauri zote nchini.

Ameongeza kuwa jukumu hilo litasimamiwa na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania. Serikali itatoza Kodi ya Majengo kwa nyumba zote kwa viwango vitakavyopangwa na Waziri na Fedha na Mipango. Nyumba ambazo hazijafanyiwa uthamini zitatozwa kwa kiwango maalum (flat rate) cha shilingi elfu kumi (10,000) kwa nyumba na shilingi elfu hamsini (50,000) kwa nyumba za ghorofa kwa kila ghorofa.

Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali itaendelea kusimamia na kuhimiza matumizi ya mashine za kielektroniki (EFDs) kwenye Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na kwa wafanyabiashara.

Ili kudhibiti mapato yatokanayo na madini, Dkt. Mpango amesema Serikali haitoruhusu usafirishaji wa madini kutoka migodini na kupeleka moja kwa moja nje ya nchi. Aidha, Serikali itaanzisha maeneo maalum (clearing houses) katika viwanja vya kimataifa, migodini, na kadhalika ambapo madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali cha kusafirisha madini hayo ambacho kitatozwa ada ya asilimia moja (clearing fee) ya thamani ya madini hayo.

Waziri huyo wa Fedha na Mipango amesema Serikali itafungua akaunti maalum (Escrow Account) kuanzia mwezi Julai 2017 ili kurahisisha na kuhakikisha kwamba marejesho ya Ushuru wa Forodha wa ziada (Additional Import Duty) wa asilimia 15 unaolipwa na waagizaji wa sukari ya viwandani yanafanyika kwa wakati. Hatua hii itaiwezesha Mamlaka ya Mapato kufanya marejesho kwa wakati kwa wazalishaji wanaotumia sukari hiyo katika kuzalisha bidhaa mbalimbali.

Katika hatua nyingine Dkt. Mpango amesititiza kuwa Serikali itaimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa kutumia vifaa na mifumo ya kielektroniki ili kuzuia uvujaji wa mapato ya Serikali.

“Mfumo uitwao “Government e-payment Gateway System” uko tayari kwa ajili ya matumizi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali. Wizara, Idara na Taasisi zote za Serikali zinaagizwa zianze kutumia mfumo huu”,  alisema Dkt. Mpango.

Amebainisha pia kuwa Serikali imezindua mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki (Electronic Revenue Collection System (e-RCS)) ambao utadhibiti udanganyifu unaofanywa na maafisa wa Serikali kwa kushirikiana na walipa kodi katika kukadiria kodi sahihi. Aidha, mfumo huu utawasaidia walipa kodi kwa kuwa na uhakika wa kiasi cha kodi wanayopaswa kulipa. Mfumo huo wa e-RCS utaanza rasmi katika mwaka huu wa fedha kwa usimamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa upande wa Bara na Bodi ya  Mapato Zanzibar (ZRB) kwa upande wa Zanzibar.

Katika mwaka 2017/18, Serikali inapanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 31,712.0. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 19,712.4 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ikijumuisha shilingi bilioni 7,205.8 za mishahara na shilingi bilioni 9,461.4 kwa ajili ya kulipia deni la umma na huduma nyinginezo. Aidha, matumizi ya maendeleo yatakuwa shilingi bilioni 11,999.6 sawa na asilimia 38 ya bajet

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi