Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kulipa Madeni ya Walimu Kabla ya Agosti, 2020
Jun 05, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53004" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi pamoja na wawakilishi mbalimbali wa Chama cha Walimu CWT kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa CWT uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo tarehe 5 Juni 2020.[/caption]

Na Immaculate Makilika- MAELEZO

Serikali imeahidi kulipa madeni ya walimu wote nchini kabla ya mwezi Agosti mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kutatua changangamoto mbalimbali zinazowakabili walimu.

Akizungumza leo jijini Dodoma, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Walimu (CWT), Rais Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa kabla ya mwezi Agosti mwaka huu, Serikali itahakikisha walimu wote watakuwa wamelipwa fedha zao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi pamoja na wawakilishi mbalimbali wa Chama cha Walimu CWT kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa CWT uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo tarehe 5 Juni 2020.

Akifafanua namna ambavyo Serikali imeendelea kulipa madeni mishahara ya walimu, Rais Magufuli alisema kuwa tangu mwezi Novemba 2015, Serikali imelipa malimbikizo ya mishahara ya jumla shilingi bilioni 115.3 ambapo shilingi bilioni 38.3 zimelipwa kwa walimu 35,805.

“Serikali imelipa madeni ya likizo na uhamisho ya jumla ya shilingi bilioni 358.1 wakiwemo walimu, ambapo kwa mwaka huu wa fedha Serikali inatarajia kuwapandisha vyeo watumishi 290, 625 wakiwemo walimu 160,548”, alisisitiza Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa moja ya vipaumbele vya Serikali hii ni kukuza na kuimarisha Sekta ya Elimu nchini, na kuongeza kuwa Serikali itaendeleza sekta hiyo hususan katika kupanua wigo na kuboresha elimu inayotolewa kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya juu, sambamba na kuendelea kuajiri walimu .

“Niwahakikishie walimu kuwa Serikali inaendelea kushughulikia changamoto zenu, baada ya kufanyika kwa zoezi la uhakiki Serikali tayari imewapandisha vyeo watumishi 306,917 na kati ya hao walimu ni 160,367 na kwenye Mwaka huu wa Fedha Watumishi 290,625 watapandishwa vyeo wakiwemo walimu 160,548” alisema Rais Magufuli.

Baadhi ya Waalimu wakifuatilia wakati wa Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Akitaja baadhi ya mambo yaliyofanyika katika kipindi cha miaka 5 ni kuboresha sekta hiyo katika uongozi wa Awamu ya Tano ni kutoa elimu bila malipo katika shule za msingi na sekondari, tangu Disemba, 2015 hadi Februari, 2020 ambapo Serikali imegharamia shilingi trilioni 1.01.

Maboresho mengine ni pampoja na kuongezeka kwa idadi ya shule za msingi kutoka 16,899 zilizokuwepo mwaka 2015 hadi shule 17,804 mwaka 2020, shule za sekondari nazo zimeongezeka kutoka 4,708 hadi 5,330 mwaka huu. Ukarabati shule kongwe za Sekondari 73 kati ya shule Kongwe 89, yamejengwa mabweni 253 na nyumba za walimu na maabara 227, tumetoa vifaa vya maabara vipatavyo 2,956 na tumepunguza tatizo la uhaba wa madawati kutoka madawati 3,024,311 mwaka 2015 hadi madawati 8,095,207 mwaka 2020.

Vilevile bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu imeongezeka kutoka shilingi bilioni 341 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi bilioni 450 mwaka 2019/2020.

Rais Magufuli aliongeza kuwa uongozi wa CWT unaomaliza muda wake umejenga uhusiano mzuri na Serikali kwani hata ilipotokea changamoto viongozi hawa walikuwa wepesi kuwatafuta viongozi wa Serikali, hii ndio sababu kubwa katika kipindi hiki hakukuwa na migogoro kama ilivyokuwa zamani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakifurahia jambo wakati  kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa CWT uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo tarehe 5 Juni 2020.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema kuwa Serikali inawakumbusha waajiri wote kuendelea kuruhusu uwepo wa vyama hivyo mahala pa kazi pia kuvitumia vyema vyama hivyo kama daraja la utatuzi wa migogoro baina ya wafanyakazi na waajiri kwani kwa kufanya hivyo tutaongeza maendeleo katika taifa .

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CWT, Deus Seif Mkutano Mkuu wa Uchanguzi una jumla ya wajumbe 1,138 ambao wameshiriki katika mkutano huo kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa watakaoongoza kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2020.

                   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi