Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kujenga Meli Kuhudumia Bandari ya Mtwara, Comoro
Jun 17, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53293" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea Bandari ya Mtwara. (Picha kutoka Maktaba)[/caption]

Na Jacquiline Mrisho - Dodoma

Serikali imeendelea na mipango yake ya kujenga meli mpya kwa ajili ya kutoa huduma kati ya Bandari ya Mtwara na Comoro na kati ya Bandari ya Kalema na karemi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ikiwa ni mojawapo ya mipango ya kuboresha usafiri wa majini.

Mpango huo umeelezwa jana Bungeni, jijini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakati akilivunja Bunge la 11.

Mbali na mpango huo, Rais Magufuli amesema Serikali inafanya upanuzi wa Bandari Kuu za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga na kuboresha usafiri wa maji kwenye Maziwa Makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa kwa kuboresha bandari zake pamoja na kujenga na kukarabati meli.

“Kwenye Ziwa Victoria tumekarabati meli tano za Mv. Victoria, Mv. Butiama, Mv. Clarias, Mv. Umoja na Mv. Wimbi; na tunaendelea na ujenzi wa meli mpya kubwa ya “Mv. Mwanza, Hapa Kazi Tu” itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo”, alisema Rais Magufuli.

Amefafanua kuwa kwenye Ziwa Victoria imejengwa chelezo kubwa kuliko zote ili kujenga na kukarabati meli na kwa upande wa Ziwa Tanganyika, meli ya mafuta ya MT. Sangara imekarabatiwa na Serikali ipo mbioni kuanza ukarabati wa MV Liemba.

Sambamba na hayo, kwenye Ziwa Nyasa imejengwa meli mpya ya kubeba abiria 200 na mizigo tani 200 na kule Zanzibar wamenunua meli kubwa mbili kwa ajili ya kutoa huduma katika Bahari ya Hindi. Aidha, vivuko vipya vimejengwa na vya zamani kukarabatiwa.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi