Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

SERIKALI KUIMARISHA UWEZO WA WALIMU WA MICHEZO
May 09, 2026
SERIKALI KUIMARISHA UWEZO WA WALIMU WA MICHEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, Akizungumza katika hafla ya usiku wa Tuzo kwa Wanamichezo zilizoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati  ya kuboresha elimu ya michezo, pamoja na kuinua uwezo wa walimu wa fani hiyo hapa nchini, ili kuhakikisha wanafunzi wanapata maarifa bora kwa maendeleo ya vipaji vyao.

Akizungumza  katika hafla ya usiku wa Tuzo kwa  Wanamichezo zilizoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)  tarehe 9 Mei, 2026, Mhe.  Makonda amesema, kuna umuhimu wa kuendelea kuwajengea walimu uwezo kupitia programu maalum za mafunzo ili waendane na mahitaji ya sasa.

Ameeleza kuwa, hatua hiyo itasaidia walimu kuelewa vizuri mbinu za ufundishaji pamoja na kuwasaidia wanafunzi kutambua vipaji vyao katika michezo  mapema.

"Serikali inalenga kuhakikisha walimu wanaopata nafasi ya kufundisha michezo  katika shule zetu wanakuwa na sifa na uelewa unaotakiwa ili kuongeza ubora wa elimu ya michezo.Tunaendelea kuboresha mazingira bora ya kazi, pamoja na motisha kwa walimu  zitakazowawezesha kufanya kazi kwa bidii" alisema Mhe. Makonda.

Ameongeza  kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na jamii pamoja na wadau mbalimbali ili kuhakikisha sekta ya michezo  inazidi kuimarika na kutoa wataalamu wenye ushindani na ubunifu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor