[caption id="attachment_7619" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo wakati wa mkutano baina ya Serikali na Wadau wa Maendeleo juu ya uboreshwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa nchini (LGDG) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mshauri wa Serikali kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) Dkt. Charles Sukule, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijazi na Mwakilishi wa Ubalozi wa China nchini Bw. Lin Zhiyong. (Picha na: Frank Shija)[/caption]
Na: Neema Mathias
Serikali yakusudia kuhuisha Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG) ili kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoibuliwa na wananchi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) nchini.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka nchi mbalimbali zinazochangia bajeti ya Serikali katika mkutano uliofanyika, Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).
[caption id="attachment_7621" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Dkt. Andrew Komba akifafanua jambo alipokuwa akiwasilisha mada wakati wa mkutano baina ya Serikali na wadau wa maendeleo juu ya uboreshwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa nchini (LGDG) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mshauri wa Serikali kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) Dkt. Charles Sukule, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijazi, Waziri wa Nchi, OR - TAMISEMI na Mwakilishi wa Ubalozi wa China nchini Bw. Lin Zhiyong.[/caption] [caption id="attachment_7622" align="aligncenter" width="742"] Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Bi. Miriam Mmbaga akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano baina ya Serikali na wadau wa maendeleo juu ya uboreshwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa nchini (LGDG) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]Mhe. Simbachaweni amesema kuwa Mfuko huo una umuhimu katika kuinua uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa, ambapo wananchi wamekua wakiibua miradi mbalimbali kama vile kujenga barabara, vituo vya Afya, Zahanati, nyumba za Walimu pamoja na madarasa, miradi ambayo imekuwa ikianzishwa na wananchi na kuendelezwa na Serikali.
“ Mfuko huu ulipoanzishwa wananchi walivutiwa sana na walifanya jitihada za kubuni na kuibua miradi mbalimbali kwani Serikali ilitenga bajeti ya fedha kusaidia miradi hiyo, lakini kuanzia miaka ya 2013 hadi 2015 miradi hiyo ilianza kuzorota na ndiyo maana kuna maboma mengi kama vile Vituo vya Afya, Madarasa na Nyumba za Waalimu ambayo hayakukamilika kutokana na mfuko huo kuzorota,” alisema Mhe. Simbachawene
[caption id="attachment_7624" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene (watatu kutoka kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijazi(wapili kutoka kushoto) wakifuatilia mada wakati wa mkutano baina ya Serikali na wadau wa maendeleo juu ya uboreshwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa nchini (LGDG) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]Aidha Mhe. Simbachawene alisema kuwa miradi hiyo imekuwa ikichangiwa na Serikali ambapo katika bajeti iliyopita ilitenga kiasi cha fedha takribani billion 156, lakini kwa mwaka huu wa fedha Serikali imetenga kiasi cha Shilingi billion 249, hivyo imeamua kuwashirikisha wadau wa maendeleo ili kuchangia mfuko wa miradi hiyo na kuhuisha miradi iliyokuwa imeachwa bila kumalizika.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imebadilisha mfumo uliokuwepo mwanzo ili kuuboresha zaidi katika kuweka na kupima mfumo mzima, lengo ni kuzifanya Halmashauri zitimize wajibu wao ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa kodi.
[caption id="attachment_7627" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa Umoja wa Jumuiya Ulaya (EU) akichangia mada wakati wa mkutano baina ya Serikali na wadau wa maendeleo juu ya uboreshwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa nchini (LGDG) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_7628" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bw. Zuberi Mhina Samataba akichangia mada wakati wa mkutano baina ya Serikali na wadau wa maendeleo juu ya uboreshwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa nchini (LGDG) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]“Wananchi wanapaswa kufahamu kuwa hakuna mtu yeyote atakayewaletea maendeleo badala yake ni wao wenyewe kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo baadae itapewa ushirikiano na Serikali, maendeleo yapo katika mikono ya wananchi wenyewe,” alifafanua Dkt. Kijaji.
Dkt. Kijaji aliongeza kuwa Watanzania wanapaswa kufuata kauli ya Mhe. Rais ya kujitegemea wenyewe hivyo Halmashauri zinapaswa kufanya kazi kwa bidii ili ziweze kujitegemea zenyewe pasipo kutegemea wadau wa maendeleo.
[caption id="attachment_7630" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Mhe.George Simbachawene akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la maendeleo Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase wakati wa mkutano baina ya Serikali na wadau wa maendeleo juu ya uboreshwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa nchini (LGDG) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]Naye Mwakilishi wa Balozi wa China nchini Bw. Lin Zhiyong amesema miradi itakayotekelezwa kupitia mfuko wa LGDG ina umuhimu mkubwa katika kuhakikisha maendeleo ya Mikoa na Serikali za Mitaa kwa ujumla kwakuwa kila mkoa umeonekana kuwa na vipaumbele katika sekta tofauti tofauti.
“Serikali za Mitaa zinapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuvutia wawekezaji, kuongeza fursa za ajira na kuongeza ushuru utokanao na miradi hiyo ili kusaidia Serikali Kuu badala ya kusubiri na kutegemea msaada kutoka Serikali Kuu,” alisema Zhiyong.
[caption id="attachment_7631" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Mhe.George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa maendeleo hapa nchini mara baada ya kumaliza mkutano baina ya Serikali na wadau wa maendeleo juu ya uboreshwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa nchini (LGDG) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mshauri wa Serikali kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) Dkt. Charles Sukule, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijazi, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la maendeleo Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase na Mwakilishi wa Ubalozi wa China nchini Bw. Lin ZhiyongWakati huohuo Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara - Mikindani, Bi. Beatrice Dominick amesema kuhuishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa(LGDG) utatoa fursa kwa Halmashauri nchini kukamilisha miradi iliyoachwa viporo.
Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG) ulianzisha mwaka 2004 lengo likiwa ni kusaidia utekelezaji wa Sera ya Ugatuzi wa Madaraka kwa Wananchi ya mwaka 1998 ambapo wananchi wanashiriki kuibua miradi ya maendeleo na Serikali inasaidia kukamilisha miradi hiyo.