Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuhakikisha Nchi Inajitosheleza kwa Chakula
Dec 29, 2023
Serikali Kuhakikisha Nchi Inajitosheleza kwa Chakula
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Litama katika kata ya Chinongwe, Ruangwa mkoani Lindi. , Desemba 29.2023.
Na Mwandishi wetu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka msisitizo katika kuendeleza Sekta ya kilimo kwenye mazao ya chakula na Biashara.

Amesema lengo ni kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa chakula na kila Mtanzania anayejishughulisha na kilimo aweze kukuza kipato chake na uchumi Taifa kwa ujumla.

Amesema hayo leo Desemba 29,2023 wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Juhudi B kwenye kata ya Chinongwe, Ruangwa mkoani Lindi.

Amesema Rais Dkt. Samia wakati wote amedhamiria kuhakikisha Tanzania inakuwa kimbilio la wengine wanaohitaji mazao “tumuunge mkono Rais wetu kwenye mapambano yake ya kukuza sekta ya kilimo, amefanya makubwa kwenye sekta ya kilimo ikiwemo kuagiza kutengwa kwa maeneo ya kilimo kwa ajili ya vijana”

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi