[caption id="attachment_38702" align="aligncenter" width="900"] Muwezeshaji wa Masuala ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Patrokil Kanje akizungumzia umuhimu wa kuibua changamoto na kuziwekea mkakati wa kuzitatua ili kuchochea ukuaji wa sekta binafsi hapa nchini.[/caption]
Na; Mwandishi Wetu
Serikali imesema itaendelea Kushirikiana na Sekta Binafsi hapa Nchini ili kuimarisha mazingira ya Biashara hivyo kuchochea ukuaji wa sekta hiyo.
Akizungumza leo Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda, Mkurugenzi wa Masoko wa Wizara hiyo Bw. Wilson Malosha amesema kuwa sekta Binafsi na sekta ya Umma zinajukumu kubwa la kuendelea kushirikiana ili kuimarisha na kukuza Biashara hapa nchini.
“Ukiwa na taarifa sahihi na zenye takwimu zitakusaidia kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati muafaka hali itakayochangia katika ustawi wa sekta Binafsi na pia kujenga utamaduni wa kubadilishana taarifa zinazokusanywa katika sekta husika ni jambo muhimu kwa ustawi wa sekta hii na ukuaji wa uchumi;” Alisisitiza Malosha
Akifafanua Bw. Malosha amesema kuwa wanachama wa sekta binafsi wanazo taarifa muhimu katika kukuza sekta hiyo hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kubadilishana taarifa za kisekta ili kuwasadia wawekezaji mbalimbali ambao wanataka kuwekeza hapa nchini.
[caption id="attachment_38703" align="aligncenter" width="900"]Mkurugenzi wa Masoko kutoka Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Bw. Wilson Malosha akisisitiza kuhusu umuhimu wa ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili kwa wanachama wa TPSF leo Jijini Dodoma.
Meneja Mradi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bi. Veneranda Sumila akizungumzia umuhimu wa warsha ya wanachama wa Taasisi hiyo leo Jijini Dodoma ikiwemo kuibua changamoto zinazowakabili wajasiriamali na kuweka mikakati ya kuzikabili.
Aliongeza kuwa kwa sasa Serikali inafanya kazi kwa karibu na sekta binafsi ili kuchochea maendeleo ya sekta binafsi hasa katika eneo la Biashara.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Valency Mutakyamirwa amesema kuwa lengo la warsha hiyo ni kuwaleta pamoja wanachama wa Taasisi hiyo ili kuwa na majadiliano ya kina yanyolenga kuibua changamoto na kuweka mikakati yakuziondoa kwa ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi.
Aliongeza kuwa warsha hiyo imelenga kuwajengea uwezo wanachama wa Taaisi ya Sekta Binafsi ili kuendelea kuongeza tija katika kukuza na kuendeleza mazingira ya Biashara nchini.
Kwa upande wake Mratibu kutoka Taasisi ya Best Dialogue Bi. Manka Kway amesema kuwa wamedhamiria kuwawezesha wajasiriamali kupata taarifa sahaihi kupitia kwenye maktaba ya mtandaoni ambayo inajumuisha taarifa mbalimbali ikiwemo tafiti na taarifa mbalimbali zinazowezesha kuimarishwa kwa mazingira ya biashara hapa nchini.
Aliongeza kuwa taarifa zilizopo katika maktaba hiyo ya mtandaoni ni pamoja na zile za sekta ya Biashara, Kilimo, Utalii, Uwekezaji, Sanaa na nyingine, lengo lake likiwa kuwasaidia wawekezaji na ukuaji wa sekta binafsi hapa nchini.
Taasisi ya Sekta Binafsi imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo kutoka katika sekta ya Umma katika kuimarisha na kuendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kutatua changamoto za kisekta ili kuendelea kuimarisha mazingira ya biashara hapa nchini.
Mratibu kutoka Taasisi ya Best Dialogue Bi. Manka Kway akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa warsha ya wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Valency Mutakyamirwa (wakwanza kulia) akisisitiza jambo kwa washiriki wa warsha ya wanachama wa Taasisi hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma.