Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuendelea Kukijengea Uwezo Chuo cha Kodi
Nov 18, 2017
Na Msemaji Mkuu

Baadhi ya Viongozi na Wahadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi wakiongozwa na kikosi cha bendi cha Jeshi la Polisi kuingia katika ukumbi wa Multipurpose katika Chuo hicho wakiwa tayari kuanza mahafali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Novemba 18, 2017.

Na Ismail Ngayonga

SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesema itaendelea kukijengea uwezo Chuo cha Usimamizi wa Kodi Nchini (ITA) ili kuhakikisha kuwa Chuo hicho kinazalisha Wataalamu bora wenye kukidhi  mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa mahafali ya kumi cha Chuo cha Kodi Nchini na kuongeza kuwa malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa Chuo hicho kinazalisha wataalamu wenye umahiri katika masuala ya forodha na kodi.

Dkt. Kayandabila alisema Serikali inatambua umuhimu wa Chuo hicho kwa ustawi wa kiuchumi na kijamii, hivyo kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaendelea kukipangia Chuo hicho bajeti ya maendeleo ili kukithi matumizi yake ya kimaendeleo ikiwemo kufanya tafiti kwa kiwango kinachohitajika.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi wakiongozwa na kikosi cha bendi cha Jeshi la Polisi kuingia katika ukumbi wa Multipurpose katika Chuo hicho wakiwa tayari kuanza mahafali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Novemba 18, 2017.

“Serikali itaendelea kushirikiana na Chuo cha Kodi kupitia Mamlaka ya Mapato kwa kuhakikisha kuwa mipango yenu hususani Mpango Mkakati wa Nne unaoanza kutekelezwa mwaka 2017/18 unatekelezwa kikamilifu kwa kuwapatia hosteli mpya za wanafunzi, upanuzi wa majengo ya ofisi za wakufunzi na ujenzi wa kampasi mpya ya Misugusugu Kibaha Mkoani Pwani” alisema Dkt. Kayandabila.

Pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Chuo hicho, Dkt. Kayandabuila aliutaka Uongozi wa Chuo hicho kuendelea kujiimarisha katika utafiti na kutoa mafunzo katika masuala ya kodi hususani sekta ya uchimbaji madini, mafuta na gesi na sekta ya fedha ili kusaidia kuongeza makusanyo ya mapato katika sekta hizo.

Akifafanua zaidi Kayandabila alisema utafiti katika sekta za madini, mafuta na gesi utasaidia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kukuza mapato ya ndani na kuongeza uwezo wa Serikali kutoa huduma za kijamii na kusimamia viwanda.

Baadhi ya Wanafunzi  wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi  (ITA) pichani wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na wageni mbalimbali waliohudhuria mahafahali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Novemba 11, 2017.

Baadhi ya Wanafunzi  wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi  (ITA) pichani wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na wageni mbalimbali waliohudhuria mahafahali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Novemba 11, 2017.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kicheere alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa Chuo hicho kinazalisha Wataalamu bora wa forodha na kodi pamoja na kupanua wigo wa ushirikiano na mataifa ya nje ikiwemo Botswana, Kenya, Burundi na Sudan Kusini.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa ITA kinazalisha wataalamu bora sambamba na kuendelea kuwa kuwa na Chuo cha Umahiri kama tulivyopendekezwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema Kicheere.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Isaya Jairo alisema tangu Chuo kilipopata usajili kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wameweza kutoa kudahili wanafunzi 6000, ambapo ili kupanua wigo wa masomo ya forodha na kodi, Chuo hicho kimepanga kushirikiana na vyuo mbalimbali vya nje ya nchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi