Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuendelea Kuboresha Mazingira ya Wafanyabiashara Nchini.
Sep 12, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_13367" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa uzinduzi wa Program ya maboresho ya usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP) leo Mjini Dodoma.

[/caption] [caption id="attachment_13364" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua Programu ya maboresho ya usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP) leo Mjini Dodoma. (Picha na Daudi Manongi)[/caption]

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuvutia wafanyabiasha wa ndani na nje ya nchi.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati akizindua awamu ya tano ya programu ya maboresho ya usimamizi wa fedha za Umma 2017/18 na 2021/22.

Akifafanua Mhe. Samia amesema kwamba katika kuhakikisha kunakuwepo na usimamizi mzuri wa fedha za umma, Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha kuwa wafanyabishara wote wanatumia mfumo wa kielekroniki kulipa kodi.

Aidha amesema kuwa Serikali itaendelea kupunguza matumizi ya fedha katika Wizara, Taasisi na Idara zake ili fedha hizo ziweze kutumika katika kuboresha huduma za jamii.

Naye, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa programu ya maboresho ya usimamizi wa fedha umeleta mafanikio makubwa ambapo umeongeza makusanyo na mapato ya Serikali Tanzania Bara na Visiwani.

“Awamu hii ya Tano ya program ya maboresho ya usimamizi wa fedha za Umma itaweka nguvu na kuimarisha ofisi za wakaguzi wa mahesabu na kutambua mapungufu yaliyopo katika ofisi hizo,” alifafanua Dkt. Mpango.

Vile vile katika awamu hii maboresho ya kazi za wakaguzi wa ndani katika Wizara, Taasisi, Idara pamoja mamlaka ya Serikali za mitaa nchini.

Maboresho ya programu ya usimamizu wa fedha za Umma ulianza mwaka 1998 ikiwa ni awamu ya kwanza ambayo ilihusisha uthibiti matumizi ya Serikali na kuchangia kukuza uchumi endelevu. Awamu ya pili ilifanyika mwaka 2004 – 2008 ambayo ilijikita katika kuboresha usimamizi wa fedha za umma kwa kutumia viwango vya kimataifa. Awamu ya tatu ilifanyika mwaka 2008 – 2012 ambayo ilihusisha katika kuhakikisha mbinu na mifumo iliyowekwa awamu ya kwanza inaoanishwa na kutumika ipasavyo kuleta matokeo yaliyokusudiwa na awamu ya nne ilikuwa mwaka 2012- 2017 ambayo ilenga katika nidhamu katika usimamizi wa fedha za umma na kutoa huduma bora kwa Umma ili kuleta maendeleo endelevu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi