Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuanza Kutekeleza Mpendekezo ya Tume Vurugu za Oktoba 29
Apr 23, 2026
Serikali Kuanza Kutekeleza Mpendekezo ya Tume Vurugu za Oktoba 29
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, atangaza kuwa Serikali itaanza mara moja kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Na George Lugeiyamu – MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwa Serikali itaanza mara moja kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza Aprili 23, 2026, Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kupokea ripoti ya tume hiyo, Rais Samia alisema hatua hiyo inalenga kurejesha na kuimarisha amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa—nguzo muhimu ya maendeleo ya nchi.

Amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha haki inatendeka kwa wote walioathirika, sambamba na kuchukua hatua kali dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na vitendo vya uvunjifu wa amani.

“Tusikubali kurubuniwa kuharibu amani na utulivu wa nchi yetu ambayo tumedumu nayo kwa muda mrefu. Tukumbuke kuwa hatuna Tanzania nyingine zaidi ya hii tuliyonayo,” amesema Rais Samia.

Katika hatua muhimu za utekelezaji , Rais ametangaza kuundwa kwa Tume ya Maridhiano ya Kitaifa itakayojumuisha wadau mbalimbali kwa lengo la kurejesha uelewano na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Aidha, amesema Serikali itafanyia kazi marekebisho ya Katiba na kuunda chombo maalum cha kuchunguza makosa ya jinai, ikiwa ni pamoja na kuwabaini na kuwachukulia hatua wote waliohusika kupanga na kutekeleza vurugu hizo.

Rais Samia pia ameeleza kuwa Serikali itashughulikia suala la miili ya waliopoteza maisha ambayo haijapatikana, pamoja na kufuatilia kwa karibu matukio ya watu waliotekwa na ambao bado hawajulikani walipo.

Kwa upande wa waathirika, Serikali itagharamia matibabu ya waliojeruhiwa, kuwapatia vifaa maalum waliopata ulemavu, na kutoa msaada kwa wajasiriamali walioathirika kiuchumi kutokana na vurugu hizo.

Rais Samia amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kulinda na kudumisha amani, haki na usalama wa wananchi wote wakati wote.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor