Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Inatambua Changamoto ya Ajira kwa Vijana Nchini
Jan 31, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Daudi Manongi,Pwani

Serikali imesema inatambua changamoto ya ajira inayowakumba vijana wengi nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akitoa taarifa ya Serikali kupitia vyombo vya habari Kibaha,Pwani.

“Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameamua kwa dhati kukabiliana na changamoto hii ambapo Serikali inafanya jitihada za kuanzisha mifuko ama vyama vya akiba na mikopo ambavyo vitasaidia kuwawezesha mitaji Wamachinga na Mamalishe  ili waweze kufanya shughuli zao za uzalishaji mali bila kikwazo,amesema Msigwa

Amesema Serikali imechukua hatua mbakimbali ikiwemo kujielekeza katika kukuza sekta isiyokuwa rasmi ambayo ina fursa nyingi za ajira ambapo imedhamiria kuwajengea mazingira mazuri wafanyabiashara wadogo (Machinga), Mamalishe na wengine kwa kuhakikisha wanaundiwa chombo kitakachowaangalia”, amesisitiza.

“Nataka kuwahakikishia Wamachinga wote, Serikali ya Awamu ya Sita itawalinda na inapanga mema mengi kwa ajili yenu, muhimu endeleeni kushirikiana na Serikali na kusikiliza viongozi wanawaelekeza nini kwa manufaa yenu”,amesema.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi