[caption id="attachment_37005" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akizungumza na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.[/caption]
Na; Mwandishi wetu
Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 iliyozinduliwa leo Jijini Dodoma imetajwa kuwa ya kihistoria na itasaidia Serikali katika kuchukua hatua stahiki kupambana na uharibifu wa mazingira.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Mussa Sima (Mb) wakati akizindua ripoti hiyo leo Jijini Dodoma amesema kuwa ripoti hiyo ni ya kuhistoria na itasaidia katika kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na uharibifu wa mazingira hapa nchini.
Matokeo yanaonesha kuwa kuna upotevu wa misitu takribani hekta 372,000 tangu mwaka 1995 hadi 2010 hivyo ni muhimu kuchukua hatua stahiki kuondokana na changamoto za uharibifu wa mazingira”. Alisisitiza Mhe. Sima.
[caption id="attachment_37006" align="aligncenter" width="843"]Akifafanua amesema kuwa ripoti hiyo inaonesha kuwa miji 10 tu ndio yenye miundo mbinu ya maji taka ambayo inanufaisha wananchi takribani asilimia 10.
Aliongeza kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto za uharibifu wa Mazingira kwanza kwa kuweka mfumo wa kisheria unaosimamia suala hilo na pia kuweka Taasisi mahususi inayosimamia masuala yote ya mazingira hapa nchini.
Pia alitoa wito kwa Wizara na Idara zinazojitegemea kutenga Bajeti kwa ajili ya vitendea kazi,uchakataji wa takwimu za mazingira katika maeneo yao ili kushiriki kikamilifu katika kutunza mazingira na kuchochea maendeleo endelevu yanayoenda sambamba na utunzaji wa mazingira.
Aliongeza kuwa Serikali kwa kuthamini umuhimu wa uwekezaji imeweka mazingira mazuri yanayowawezesha wawekezaji kupata cheti cha Tathmini ya mazingira ndani ya siku 70 kutoka siku 149 za awali ili kuharakisha mchakato wa uwekezaji na kuvutia wawekezaji.
[caption id="attachment_37007" align="aligncenter" width="900"]Pia aliwataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutenga maeneo ya uwekezaji na kuyapima ili wawekezaji wanapojitokeza wapatiwe maeneo hayo yakiwa yamepimwa ili kuharakisha maendeleo.
Uzinduzi wa Ripoti ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 ni kichocheo cha maendeleo kwa kuwa inatoa taswira halisi ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kulinda mazingira na kutekeleza miradi yote kwa kuzingatia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake.
[caption id="attachment_37008" align="aligncenter" width="900"]