Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda ampokea Nyota wa zamani wa Leeds, Manchester United na England Bw. Rio Ferdinand, ambaye amewasili nchini leo Mei 19, 2026, kwa ziara ya siku nne ya mwaliko wa Mhe. Makonda.

Katika mapokezi hayo, Mhe. Makonda aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa na Viongozi wengine wa Wizara hiyo
Katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 3, maelf ya mashabiki wa soka wamejitokeza kumlaki nyota huyo wa zamani ambaye amesema hakutegemea kupata mapokezi makubwa namna hiyo.

"Tanzania ni nchi nzuri sana, nimepata mapokezi makubwa, sikutegemea kupata mapokezi namna hii, nitawaonesha watu uzuri wa Tanzania na vivutio vyake" amesema Nyota huyo.
Nae Waziri Makonda amesema ujio wa mgeni huyo ni faraja kubwa kwa nchi kwani kutaitangaza Tanzania katika nyanja za burudani na Utalii masuala ambayo Serikali ya Dktw. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa akiyaunga mkono.

Ziara ya Ferdinand inatajiwa kujumuisha shughuli mbalimbali ikiwepo kutembembelea vituo vya michezo vya Vijana (Academies), kukutana na wadau wa michezo pamoja na shughuli za Utalii.